Page 46 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 46
Sura ya Tano
Sura ya Tano
Mazoezi ya viungo
Mazoezi ya viungo
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Mazoezi ya viungo hufanyika kwa malengo mbalimbali ikiwemo
mtindo wa maisha wenye kujenga afya. Katika sura hii, utajifunza
namna ya kufanya mazoezi ya viungo ya uratibu na unyumbufu
wa mwili. Umahiri utakaoujenga utakusaidia kuimarisha stadi za
uchezaji wa michezo na kujenga afya na utimamu wa mwili.
Fikiri
Mazoezi ya viungo ya uratibu na unyumbufu wa mwili.
Mazoezi ya viungo ya uratibu na unyumbufu wa mwili
Kuna aina mbalimbali za mazoezi ya viungo kwa ajili ya kujenga
uratibu na unyumbufu wa mwili. Mazoezi haya yanaweza kufanywa
na mtu mmoja mmoja, wawili wawili au kikundi na kwa mitindo
tofauti tofauti. Baadhi ya mazoezi hayo ni koni mzunguko kwa ajili
ya kujenga unyumbufu wa mwili na kuweka puto hewani kwa ajili ya
kujenga uratibu wa mwili.
Koni mzunguko
Hili ni zoezi la viungo linalobeba aina mbalimbali za mazoezi ya
unyumbufu.
Vifaa:
(a) Koni sita; na
(b) Mazulia ya mazoezi
39
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 39
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 39 19/10/2024 16:35