Page 44 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 44
Hatua za kufinyanga kwa njia ya bapa na pindi
(a) Chagua umbo unalotaka kufinyanga. Inaweza kuwa bakuli
au chombo cha kupandia maua;
(b) Andaa udongo kwa kuzingatia mahitaji ya kifani unachotaka
FOR ONLINE READING ONLY
kufinyanga;
(c) Amua ni maumbo yapi yawe bapa na yapi yawe pindi; kisha
(d) Anza kufinyanga kwa hatua ya bapa au pindi kulingana na
muundo wa umbo la kifani unachotaka kufinyanga.
Kukausha kifani
Kifani kilichofinyangwa kinapaswa kukaushwa kwa upepo au moto
kulingana na asili ya udongo ili kiwe imara, kisha kitawekwa nakshi ili
kipendeze. Endapo kifani hakitakauka vizuri hakitafaa kwa matumizi
ya muda mrefu.
Hatua za kukausha kifani
(a) Baada ya kumaliza kufinyanga kifani, kianike juani kwa
muda mfupi;
(b) Weka nakshi unayoipenda kwa mfano maua na mistari; na
(c) Kianike kivulini ili kikauke taratibu.
Zoezi
1. Eleza namna ya kuandaa udongo wa mfinyanzi kwa ajili ya
kufinyanga vyungu.
2. Je, ni njia gani inafaa kufinyanga kifani cha mitungi?
37
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 37 19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 37