Page 32 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 32
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 3: Picha njiti ya kitanda
Kazi ya kufanya namba 2
(a) Tumia penseli na karatasi kuchora angalau picha tano za
njiti kuonesha vitu vitano vinavyopatikana katika mazingira
ya shuleni au nyumbani;
(b) Onesha picha hizo darasani kwa ajili ya majadiliano; na
(c) Tunza picha hizo kwa ajili ya maonesho ya sanaa shuleni.
Matumizi ya mistari katika kuchora picha za vitu mbalimbali
kwa penseli
Matumizi ya mistari ni muhimu sana katika sanaa ya uchoraji kwa
panseli. Zifuatazo ni hatua za msingi za kufuata katika kuchora
michoro ya vitu mbalimbali:
(i) Chagua penseli sahihi. Tumia penseli za aina tofauti
kama vile HB, 2B, na 4B. Penseli za HB ni nzuri kwa
kuchorea mistari ya myepesi, wakati 2B na 4B ni bora
kwa kukoleza mistari;
(ii) Anza kwa kuchora mistari itakayokuongoza. Chora
mistari ya mwongozo ili kupata uwiano sahihi wa mchoro
wako. Mistari hii inapaswa kuwa miepesi ili iwe rahisi
kufuta baadaye;
25
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 25
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 25 19/10/2024 16:35