Page 27 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 27
(ii) Anza kwa kuchora maumbo rahisi. Chora maumbo
mbalimbali kama vile duara, miraba, na mistari ambayo
inajenga msingi wa michoro mingine.
(iii) Chora mistari myepesi ya mchoro wa kitu unachotaka
kuchora. Hii itakusaidia kufuta na kurekebisha kwa
FOR ONLINE READING ONLY
urahisi.
(iv) Koleza mchoro wako. Tumia penseli kukoleza mchoro
wako ili uweze kuonekana vizuri.
(v) Pitia upya mchoro wako. Unatakiwa kupitia upya mchoro
uliouchora ili kuboresha mistari kwa kufuta alama zisizo
za lazima ili kuboresha mwonekano wa jumla.
Matumizi ya mistari katika kuchora picha njiti
Picha njiti ni taswira za watu au vitu zinazochorwa kwa mstari
pekee. Mistari hiyo ni kama vile mistari ya ulalo, wima na iliyopinda.
Huu ni uchoraji wa awali kwa yeyote anayeanza kujifunza uchoraji.
Kielelezo namba 1 kinaonesha picha njiti zilizochorwa kwa kutumia
penseli.
Kielelezo namba 1: Picha njiti mbalimbali
Vifaa vya kuchorea
Vifuatavyo ni baadhi ya vifaa ambavyo hutumika katika kuchora
picha njiti:
(i) Penseli;
(ii) Kichongeo cha penseli;
20
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 20
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 20 19/10/2024 16:35