Page 26 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 26
Sura ya Tatu
Sura ya Tatu
Uchoraji
FOR ONLINE READING ONLY
Uchoraji
Utangulizi
Sanaa ya uchoraji hutumia michoro kama lugha iliyokamilika
ambayo watu wanaweza kuiona na kuielewa hata kama hawajui
kusoma na kuandika. Katika sura hii, utajifunza kuchora picha
za vitu mbalimbali kwa kutumia penseli. Umahiri utakaoujenga
utakuwezesha kuchora picha za vitu mbalimbali kwa ustadi.
Fikiri
Jinsi ya kuchora picha za vitu kwa penseli.
Kuchora picha za vitu mbalimbali kwa kutumia penseli
Kuchora picha kwa kutumia penseli ni sanaa inayohusisha matumizi
ya penseli kuunda picha au michoro. Vifaa vinavyohitajika ni penseli
za aina mbalimbali kama vile HB, 2B na 4B, karatasi ya kuchora, na
kifutio.
Hatua za kuzingatia katika kuchora picha za vitu mbalimbali
kwa kutumia penseli
(i) Andaa vifaa vya kuchorea. Utahitaji vifaa mbalimbali
vya kuchorea kama vile, karatasi, ubao wa kuegemezea
karatasi, kifutio, kichongeo na penseli za aina mbalimbali
kama vile HB, 2B and 4B.
19
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 19
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 19 19/10/2024 16:35