Page 28 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 28
(iii) Karatasi;
(iv) Kifutio;
(v) Meza na kiti;
(vi) Kibao cha kuchorea; na
FOR ONLINE READING ONLY
(vii) Kibanio cha kubania karatasi
Kanuni za uchoraji wa picha njiti
Ili kuchora picha njiti, kanuni zifuatazo ni muhimu kuzingatiwa:
1. Picha njiti ichorwe kwa kuzingatia ujumbe husika;
2. Fikiria wazo la kitu utakachochora au andaa kitu halisi
kitakachochorwa;
3. Zingatia matumizi mbalimbali ya mistari ili kupata uhalisia wa
jambo;
4. Anza kuchora kwa kutumia mistari myepesi;
5. Tumia kifutio kwa uangalifu ili usichafue mchoro; na
6. Usitumie kalamu ya wino kuchorea picha katika hatua hii.
Hatua za kuzingatia katika kuchora picha njiti
Katika kuchora picha njiti, zipo hatua ambazo unatakiwa kuzizingatia
ili picha yako ilete maana. Hatua hizo ni:
(a) Chagua au buni vitu unavyotaka kuchora;
(b) Andaa karatasi na penseli ya kuchorea;
(c) Anza kuchora picha njiti kwa kutumia mistari myepesi;
(d) Rekebisha kama kuna sehemu ambayo umekosea kwa
kutumia kifutio;
(e) Koleza mistari baada ya kuwa umepata umbo sahihi; na
(f) Ondoa mistari isiyotakiwa pamoja na uchafu uliosababishwa
na ufutio.
21
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 21
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 21 19/10/2024 16:35