Page 21 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 21
Kuimba kwa kuzingatia toni
Toni ni sauti yenye kipimo maalumu na ubora inayotokana na noti
ya muziki au sauti ya mtu. Katika kuimba, ni muhimu kuzingatia
toni sahihi kwa kila neno na sentensi. Ili wimbo uwe na ubora
unaotakiwa, kila neno linapaswa kuimbwa kwa toni yenye maana na
FOR ONLINE READING ONLY
kuelezea hisia za wimbo. Matumizi sahihi ya toni yanaongeza uzuri
na ubora wa sauti. Hivyo, mwimbaji, anapaswa kufanya mazoezi
ya kuimba kwa kuzingatia toni na kuhakikisha anawasilisha wimbo
kwa umahiri na hisia. Kuna mambo mbalimbali ambayo mwimbaji
anapaswa kuyazingatia ili kutoa sauti yenye ubora. Mambo hayo ni
kama:
(a) Mkao sahihi wakati wa uimbaji. Mwimbaji anapaswa
kuhakikisha anauweka mwili wake katika hali ya usawa ikiwa
ni pamoja na shingo kuwa wima, mabega na mikono kuwa
huru, kifua na tumbo kutokazwa, na miguu kuachanishwa
kidogo;
(b) Upumuaji sahihi wakati wa uimbaji. Ili kuweza kupumua kwa
usahihi wakati wa kuimba, mwimbaji anatakiwa kufanya
mazoezi ya pumzi. Kwa mfano, kuvuta hewa na kuitunza kwa
muda na kisha kuitoa taratibu; na
(c) Matamshi sahihi wakati wa uimbaji. Matamshi sahihi ni muhimu
katika kupata toni sahihi wakati wa kuimba. Pia, humsaidia
mwimbaji kuzalisha sauti inayofanya maneno yasikike vizuri.
Vilevile, kuboresha ubora wa sauti. Hivyo, kuunda toni
ambayo inavutia wasikilizaji na kuhakikisha ujumbe wa wimbo
unaeleweka kwa urahisi.
Kazi ya kufanya namba 2
Imba wimbo wa shule yako kwa kuzingatia toni sahihi.
14
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 14
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 14 19/10/2024 16:35