Page 14 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 14
Zoezi la kwanza
1. Bainisha faida za kufanya mazoezi ya miondoko ya mwili
katika uigizaji.
2. Taja baadhi ya hatua utakazofuata wakati wa kuigiza miondoko
FOR ONLINE READING ONLY
mbalimbali ya wanyama.
Mazoezi ya hisia katika uigizaji
Mazoezi ya hisia ni mazoezi ambayo yanamsaidia mwigizaji
kuchunguza, kuelewa na kumudu hisia mbalimbali kwa ufanisi
katika uigizaji. Mifano ya hisia ni kama vile furaha, huzuni, hasira,
hofu, kushangaa, aibu, chuki, upendo na wivu. Mwigizaji anaweza
kufanya mazoezi ya hisia kwa njia mbalimbali ikiwemo kumbukumbu
za hisia na mazoezi ya kucheka au kulia.
Kumbukumbu za hisia. Mwigizaji anaweza kutumia kumbukumbu za
hisia kutokana na matukio ya maisha yake mwenyewe. Hii husaidia
kuamsha hisia zinazohitajika wakati wa kuigiza tabia fulani. Mbinu
hii humsaidia mwigizaji kuleta uhalisia katika uigizaji. Mara nyingi
hisia hizi hutokana na uzoefu wake binafsi.
Kazi ya kufanya namba 4
Fikiri kuhusu tukio ambalo lilileta furaha au huzuni kubwa
maishani mwako. Kisha, tumia vitendo kuonesha hisia zako.
7
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 7
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 7 19/10/2024 16:35