Page 9 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 9
na uigizaji kwa hisia. Mfano wa miondoko ya mwili ni kama vile
kutembea, kusimama au kucheza ngoma. Hii inajumuisha lugha
ya mwili, ishara na namna ya kutembea au kusimama. Mwigizaji
huweza kutumia miondoko ya mwili kuelezea hisia kama furaha,
huzuni, hofu au kujiamini. Sanaa kama vile michezo ya kuigiza na
FOR ONLINE READING ONLY
ngoma mara nyingi hutumia miondoko ya mwili ili kuwasiliana na
watazamaji.
Mifano ya miondoko ya mwili katika uigizaji
Miondoko ya mwili katika uigizaji husaidia mwigizaji kufanya hadhira
ielewe uhusika wake na ujumbe. Ifuatayo ni mifano ya miondoko ya
mwili katika uigizaji:
(a) Kusimama wima. Mwigizaji anaposimama wima na kifua
mbele anaweza kuwa anaonesha kujiamini, kuwa na
mamlaka, nguvu au ujasiri;
(b) Kuangalia chini. Mwigizaji anapoangalia chini au kukwepa
macho ya wengine huonesha hisia za kutojiamini, kuogopa,
aibu, hatia au unyonge;
(c) Kukunja mikono kifuani. Miondoko hii huonesha kuwa
mwigizaji anajihami, kutokuwa tayari kwa mazungumzo
au hisia za kutokuwa na uhakika. Vilevile, miondoko hii
inaweza kuashiria hasira au ukali wa mwigizaji;
(d) Kutembea kwa haraka na hatua fupi. Hii katika uigizaji
huonesha wasiwasi, hofu au haraka. Mwigizaji huonesha
kuwa ana mambo mengi anayoyawaza au anajaribu
kikimbia hali au tukio fulani;
(e) Kutikisa kichwa juu chini kwa upole. Katika uigizaji hii
inaweza kuonesha kukubali au kuridhia jambo au kitu.
Mwigizaji anapotikisa kichwa kwa upole anaonesha
kwamba anakubaliana na mawazo au pendekezo la mtu
mwingine;
2
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 2
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 2 19/10/2024 16:35