Page 8 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 8
Sura ya Kwanza
Sura ya Kwanza
Uigizaji
Uigizaji
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Uigizaji ni mojawapo ya sanaa inayofikisha ujumbe kwa jamii
kwa kutumia maneno na matendo. Katika sura hii, utafanya
mazoezi ya miondoko ya mwili, hisia na sauti kwa kuigiza viumbe
hai na visivyo hai. Umahiri utakaoujenga utakuwezesha kufanya
maigizo mbalimbali kwa ustadi na kwa kujiamini ili kuelimisha na
kuburudisha jamii.
Fikiri
Miondoko ya mwili katika uigizaji.
Mazoezi ya uigizaji
Mazoezi ya uigizaji hujumuisha maandalizi ya mbinu mbalimbali za
kimwili na kiakili. Mwigizaji huyafanya maandalizi haya kwa ajili ya
kujenga na kuelewa vizuri tabia na hisia za uhusika anaopaswa
kuigiza. Hii hufanya onyesho la kuigiza kuwa bora zaidi. Mazoezi ya
uigizaji hujumuisha miondoko ya mwili, kuigiza aina mbalimbali za
hisia na utoaji wa sauti.
Mazoezi ya miondoko ya mwili katika uigizaji
Miondoko ya mwili katika uigizaji ni namna mwigizaji anavyotumia
mwili wake kuwasilisha ujumbe fulani bila kutumia maneno. Miondoko
ya mwili hujulikana kama ni mawasiliano kwa kutumia vitendo. Pia,
miondoko ya mwili hujumuisha uigaji, uigizaji mjongeo na mgando
1
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 1
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 1 19/10/2024 16:35