Page 12 - Sanaa_Michezo_Drs_4
P. 12
Kazi ya kufanya namba 2
Tumia miondoko ya mwili na sauti kuigiza mienendo ya paka,
nyani, kuku na simba.
FOR ONLINE READING ONLY
Mifano ya uigizaji wa miondoko ya viumbe visivyo hai
Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya namna ya kuigiza miondoko ya
mwili ya viumbe visivyo hai:
1. Kuigiza miondoko ya baiskeli. Kwa kutumia mikono na miguu,
weka mikono yako mbele kama vile unashika usukani wa
baiskeli. Piga magoti kidogo na uanze kusogeza miguu yako
kama vile unakanyaga pedali. Kwa kutumia mwili, inama mbele
kidogo na ugeuze mwili wako upande kwa upande kama vile
dereva anavyogeuza baiskeli;
2. Kuigiza miondoko ya gari. Kwa kutumia mikono, shika mbele
kama vile unashika usukani wa gari. Geuza usukani kwa mikono
yako kama vile unavyogeuza usukani wa gari. Tumia mguu
mmoja kama vile unakanyaga kichapuzi mafuta na mwingine
breki;
3. Kuigiza miondoko ya pikipiki. Shika mikono yako mbele kama
vile unashika usukani wa pikipiki kisha kwa kutumia miguu piga
kiki kama unawasha pikipiki, geuza usukani kwa mikono yako
na uanze kuzungusha mikono yako kama vile unavyogeuza
pikipiki. Inama mbele kidogo na ugeuze mwili wako upande
kwa upande kama unavyogeuza pikipiki; na
4. Kuigiza miondoko ya mawe. Shika kitu mkononi chenye ukubwa
wa jiwe dogo ambalo unaweza kulisukuma kwa mkono wako.
Weka chini, kisha tumia mguu wako kulisogeza sehemu moja
kwenda nyingine.
Vilevile, unaweza kuigiza miondoko ya vitu vingine kama vile:
1. Miondoko ya mto. Tembea taratibu huku mikono yako
ukiiyumbisha mithili ya mawimbi ya maji;
5
19/10/2024 16:35
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 5
SANAA NA MICHEZO BALANCING.indd 5 19/10/2024 16:35