Page 6 - SayansiStd4
P. 6
Utangulizi
Kitabu cha Sayansi kimetayarishwa kwa kuzingatia muhtasari
wa somo la Sayansi Elimu ya Msingi Darasa la III-VI uliotolewa
na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia mwaka 2023. Baadhi
FOR ONLINE READING ONLY
ya maudhui ya kitabu hiki yamechukuliwa kutoka katika vitabu
vya Sayansi na Teknolojia Darasa la Tatu, Nne, Tano, Sita
na Saba. Vitabu hivyo vilichapishwa mwaka 2018 na Darasa
la Saba mwaka 2021 kwa kuzingatia muhtasari wa Somo la
Sayansi na Teknolojia wa mwaka 2016. Kitabu hiki kina sura
sita ambazo ni Kanuni za afya, Magonjwa, Maada, Uunguaji
wa vitu, Nishati na Usimbaji katika kompyuta.
Maudhui ya kitabu hiki yamewasilishwa kwa njia ya matini, kazi
za kufanya, majaribio, mazoezi, michoro na picha mbalimbali
ili kukuwezesha kujenga umahiri uliokusudiwa katika kila
sura. Kila sura ina kazi za kufanya na mazoezi ya kutosha
yatakayokuwezesha kupima uelewa wako kuhusu maudhui
husika. Unatakiwa kufanya kazi zote, majaribio, maswali na
mazoezi peke yako au kwa kushirikiana na wenzako.
Aidha, unashauriwa kuwashirikisha walimu, wazazi au walezi
unapotumia maktaba, mtandao au vyanzo vingine kutafuta
taarifa. Jifunze zaidi kupitia maktaba mtandao
https://ol.tie.go.tz au ol.tie.go.tz
Taasisi ya Elimu Tanzania
v
14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 5
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 5 14/01/2025 18:38