Page 8 - SayansiStd4
P. 8
Sura ya Kwanza
Kanuni za afya
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Afya bora ni msingi imara katika maisha. Katika sura hii,
utajifunza kuhusu kanuni za afya zikiwemo mlo kamili,
mazoezi ya mwili, usafi wa mazingira, alama na taarifa
muhimu. Umahiri utakaoujenga utakuwezesha kuzingatia
kanuni za afya. Vilevile, utaweza kuchukua tahadhari stahiki
katika kulinda usalama wako na wa watu wengine.
Mambo unayoweza kufanya kila siku
Fikiri
ili kutunza afya
Dhana ya kanuni za afya
Kuzingatia kanuni za afya ni jambo la muhimu ili kudumisha
afya bora. Afya bora ni hali ya kuwa imara kimwili na kiakili. Ili
kuwa na afya bora ni lazima kuzingatia kanuni za afya. Miongoni
mwa kanuni hizo ni kula mlo kamili na kufanya mazoezi ya
mwili. Vilevile, kuzingatia usafi wa mwili na mazingira. Kanuni
nyingine za kuzingatia ni alama na taarifa muhimu katika
mazingira. Kielelezo namba 1 kinaonesha mifano ya kanuni
za afya.
1
14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 1
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 1 14/01/2025 18:38