Page 12 - SayansiStd4
P. 12
misuli na mifupa ya mwili.Vitamini na madini hupatikana
katika mbogamboga kama vile kabichi, sukumawiki, mchicha,
biringanya na karoti. Pia, hupatikana katika matunda mfano
papai, chungwa, parachichi, zabibu na embe. Kielelezo namba
FOR ONLINE READING ONLY
5 kinaonesha mifano ya vyakula vyenye vitamini na madini.
Kielelezo namba 5: Vyakula vyenye vitamini na madini
Maji
Maji si sehemu ya makundi makuu ya vyakula yanayounda
mlo kamili. Hatahivyo, mwili huhitaji maji ya kutosha ili
uweze kufanya kazi ipasavyo. Hii ni kwa sababu yana madini
mbalimbali yanayosaidia mifumo ya mwili kufanya kazi vizuri.
Kwa mfano, umeng’enywaji wa chakula na ufyonzwaji mzuri wa
virutubisho kutoka kwenye vyakula. Pia, maji husaidia kuondoa
takamwili na sumu mwilini. Vilevile, maji husaidia kurekebisha
joto la mwili.
Kazi ya kufanya namba 3
1. Pangilia mlo kamili wa mchana kwa kutumia vyakula
vinavyopatikana katika maeneo yako.
2. Eleza umuhimu wa kila aina ya chakula iliyojumuishwa
kwenye mlo wako.
5
14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 5
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 5 14/01/2025 18:38