Page 11 - SayansiStd4
P. 11
FOR ONLINE READING ONLY
(a) Vyakula vyenye kabohaidreti (b) Vyakula vyenye mafuta
Kielelezo namba 3: Vyakula vyenye virutubisho vya kabohaidreti na
mafuta
Vyakula vya kujenga mwili
Vyakula vya kujenga mwili ni vyenye virutubisho vya protini.
Vyakula hivyo ni kama vile samaki, maziwa, nyama, mayai,
njegere na maharage. Kazi ya vyakula hivi ni kujenga mwili na
kuufanya ukue vizuri. Pia, vyakula hivi hutumika kutengeneza
seli mpya ili kuchukua nafasi ya seli zilizozeeka au kufa.
Kielelezo namba 4 kinaonesha vyakula vya kujenga mwili.
Kielelezo namba 4: Vyakula vya kujenga mwili
Vyakula vya kulinda mwili
Vyakula vya kulinda mwili ni vyenye vitamini na madini.
Vyakula hivi husaidia kuimarisha afya na kuwezesha mwili
kujikinga na magonjwa. Pia, husaidia kujenga na kuimarisha
4
14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 4
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 4 14/01/2025 18:38