Page 14 - SayansiStd4
P. 14
Vijanabalehe
Hili ni kundi lililopo katika kipindi cha balehe. Katika kipindi
hiki mwili hupitia mabadiliko na kukua kwa haraka, hivyo
kijana huhitaji mlo wenye vyakula vya kutosha vya kujenga,
FOR ONLINE READING ONLY
kulinda na kuupa mwili nguvu na joto. Katika umri huu, kijana
hujishughulisha na shughuli mbalimbali kama vile michezo,
kulima au kusoma kwa muda mrefu. Hivyo, ni muhimu mlo wa
kijana uwe na kiwango kikubwa cha vyakula vya kuupa mwili
nguvu. Hii ni kwa sababu mwili unahitaji nguvu za kutosha
kuzimudu shughuli zake. Kielelezo namba 7 kinaonesha mlo
kamili wa kijanabalehe.
Vyakula vya
kuupa mwili
Vyakula nguvu
vya kujenga
mwili
Vyakula vya
kulinda mwili
Kielelezo namba 7: Mlo kamili wa kijanabalehe
Wazee
Kinga ya mwili hupungua katika kipindi cha uzee. Hivyo,
wazee wanatakiwa kula vyakula vyenye vitamini ili kujikinga na
magonjwa ya mara kwa mara. Pia, wanapaswa kula vyakula
vyenye madini mbalimbali ili kuimarisha mifupa, na misuli ya
mwili. Vilevile, wanatakiwa kula kiasi kidogo cha vyakula vya
7
14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 7 14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 7