Page 18 - SayansiStd4
P. 18
4. Nini kitatokea usipokula mlo kamili?
5. Fafanua umuhimu wa vyakula vya kujenga na kulinda
mwili kwa mgonjwa.
FOR ONLINE READING ONLY
Mazoezi ya mwili
Mazoezi ya mwili ni muhimu ili kujenga afya bora. Mazoezi ya
mwili ni kama vile kucheza mpira wa miguu, kukimbia, kuruka
viunzi na kutembea. Kielelezo namba 11 kinaonesha wanafunzi
wakifanya mazoezi ya mwili.
Kielelezo namba 11: Wanafunzi wakicheza mpira
Kazi ya kufanya namba 5
Tumia maktaba, matini mtandao au vyanzo vingine vya
taarifa, kutafuta taarifa kuhusu mazoezi ya mwili. Kisha,
fanya mazoezi ya mwili unayoyamudu.
11
14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 11
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 11 14/01/2025 18:38