Page 20 - Sayansi_Drs_4
P. 20
Usafi wa mwili na mavazi
Usafi wa mwili na mavazi ni muhimu kwa afya zetu. Mwili na
mavazi visafishwe kwa kutumia vifaa maalumu ili kuepuka
magonjwa. Usafi wa mwili unahusisha kinywa, ngozi, nywele,
FOR ONLINE READING ONLY
kucha na mavazi.
Usafi wa kinywa
Kinywa kinapaswa kusafishwa kwa kutumia mswaki, dawa
ya meno na maji safi na salama. Kupiga mswaki husaidia
kuondoa mabaki ya chakula kwenye meno. Mabaki hayo
yakibaki, bakteria waliopo kinywani huyatumia kama chakula na
kuzalisha tindikali. Tindikali hiyo huharibu meno na kuyafanya
yatoboke. Ni muhimu kupiga mswaki angalau mara mbili kwa
siku. Piga mswaki asubuhi unapoamka na usiku kabla ya kulala.
Hii husaidia meno yako kubaki na afya nzuri.
Kazi ya kufanya namba 6
1. Tumia maktaba, matini mtandao au vyanzo vingine
kutafuta taarifa kuhusu utunzaji wa kinywa.
2. Shirikisha taarifa ulizozipata kuhusu utunzaji wa kinywa
kwa wanafunzi wenzako kwa ajili ya majadiliano.
Kuoga
Tunapaswa kuoga kwa kutumia maji safi na sabuni kila siku.
Inashauriwa kuoga asubuhi baada ya kuamka na jioni kabla
ya kulala. Hii husaidia kuepuka magonjwa ya ngozi na harufu
mbaya. Pia, uso unapaswa kuoshwa kwa maji safi na sabuni
ili kuondoa tongotongo na kujikinga na magonjwa ya macho.
13
05/11/2024 14:50
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 13 05/11/2024 14:50
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 13