Page 19 - SayansiStd4
P. 19
Faida za kufanya mazoezi ya mwili
Inashauriwa kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara. Kufanya
mazoezi ya mwili mara kwa mara husaidia yafuatayo:
FOR ONLINE READING ONLY
(a) Kuwa na afya bora;
(b) Kurekebisha utendaji wa mifumo ya mwili kama vile mfumo
wa mzunguko wa damu, mmeng’enyo wa chakula na utoaji
takamwili;
(c) Kuimarisha kinga ya mwili ili kupambana na magonjwa
mbalimbali;
(d) Kuondoa msongo wa mawazo na sonona; na
(e) Kuchangamsha ubongo na kuburudika.
Madhara ya kutofanya mazoezi ya mwili
Kutofanya mazoezi ya mwili husababisha madhara yafuatayo:
(a) Kuwa na afya duni na dhaifu;
(b) Uzito wa mwili unaweza kuongezeka kupita kiasi, hivyo
kuwa kwenye hatari ya kupata kiribatumbo;
(c) Kupata magonjwa yanayoambatana na uzito mkubwa
kama vile shinikizo la damu, kisukari na matatizo ya moyo;
(d) Kupata msongo wa mawazo na sonona; na
(e) Udhaifu wa misuli na mifupa.
Usafi wa mwili na mazingira
Usafi wa mwili na mazingira ni muhimu ili kuwa na afya bora.
Miili yetu inapaswa kuwa safi wakati wote. Pia, mavazi na
maeneo yanayotuzunguka yanapaswa kuwa safi kwa wakati
wote.
12
14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 12
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 12 14/01/2025 18:38