Page 15 - SayansiStd4
P. 15
kuupa mwili nguvu . Hii itawasaidia kupata nguvu za kufanyia
shughuli mbalimbali na kuwaepusha kupata uzito mkubwa wa
mwili. Aidha, wazee wanatakiwa kula vyakula vya kujenga mwili.
Vyakula hivi huwasaidia wazee kurejesha chembechembe hai
FOR ONLINE READING ONLY
na tishu zilizokufa. Kielelezo namba 8 kinaonesha mlo kamili
wa mzee.
Vyakula
vya kujenga
mwili
Vyakula
vya kulinda
mwili
Vyakula vya
kuupa mwili
nguvu na
joto
Kielelezo namba 8: Mlo kamili wa mzee
Watu wanaofanya kazi zinazotumia nguvu nyingi
Watu wanaofanya kazi zinazotumia nguvu nyingi ni kama vile
wabeba mizigo au makuli, waendesha mikokoteni, mafundi
magari na wajenzi. Kundi hili, hutakiwa kula kiasi kikubwa cha
vyakula vya kuupa mwili nguvu. Vyakula hivi huupa mwili nguvu
za kutosha kufanya kazi nzito. Pia, wanapaswa kunywa maji
ya kutosha ili kusaidia umeng’enywaji wa haraka wa chakula.
Hii itasaidia kuupatia mwili nguvu na kurejesha maji mwilini
yanayopotea kwa njia ya jasho wanapofanya kazi. Kielelezo
namba 9 kinaonesha mlo kamili wa mtu anayefanya kazi za
kutumia nguvu nyingi.
8
14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 8 14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 8