Page 10 - SayansiStd4
P. 10
Vyakula vya
FOR ONLINE READING ONLY
Vyakula vya kuupa mwili
kulinda mwili nguvu
Vyakula vya
kujenga mwili
Kielelezo namba 2: Mfano wa makundi makuu ya vyakula katika mlo
kamili
Kazi ya kufanya namba 2
1. Bainisha vyakula mbalimbali vinavyopatikana katika
mazingira yako.
2. Ainisha vyakula hivyo katika makundi makuu sahihi.
Vyakula vya kuupa mwili nguvu
Vyakula vya kuupa mwili nguvu ni vyenye virutubisho vya
wanga au kabohaidreti pamoja na mafuta.Vyakula vyenye
kabohaidreti ni kama vile mahindi, viazi, mihogo, ndizi, wali
na mkate. Vyakula vyenye mafuta ni kama vile nazi, karanga,
mafuta na parachichi. Vyakula hivi huuwezesha mwili kuwa
na uwezo wa kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo kucheza,
kulima na kutembea.Vilevile, mafuta husaidia kuupa mwili
joto. Kielelezo namba 3 kinaonesha mifano ya vyakula vyenye
virutubisho vya kabohaidreti na mafuta.
3
14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 3 14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 3