Page 9 - SayansiStd4
P. 9
FOR ONLINE READING ONLY
(a) Kufanya mazoezi ya mwili (b) Kula mlo kamili
Kielelezo namba 1: Kuzingatia kanuni za afya
Kazi ya kufanya namba 1
Tumia maktaba, matini mtandao au vyanzo vingine vya taarifa
kutafuta taarifa kuhusu kanuni za afya. Wasilisha taarifa hizo
darasani kwa ajili ya majadiliano.
Mlo kamili
Mlo kamili ni mlo wenye virutubisho vyote vya chakula katika
uwiano sahihi. Mlo kamili huundwa na vyakula kutoka katika
makundi makuu matatu. Mosi ni vyakula vya kuupa mwili nguvu.
Vyakula hivyo vina virutubisho vya kabohaidreti au wanga. Pili,
ni vyakula vya kujenga mwili vyenye virutubisho vya protini.
Mwisho ni vyakula vya kulinda mwili vyenye virutubisho vya
vitamini na madini. Mlo kamili hutupatia virutubisho vyote muhimu
ambavyo mwili unahitaji kwa uwiano sahihi. Umuhimu wa mlo
kamili ni kuimarisha kinga ya mwili ili kuweza kupambana na
magonjwa. Kielelezo namba 2 kinaonesha mfano wa makundi
makuu ya vyakula katika mlo kamili.
2
14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 2
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 2 14/01/2025 18:38