Page 13 - SayansiStd4
P. 13
Mlo kamili kwa makundi mbalimbali ya watu
Mahitaji ya vyakula ni tofauti kwa kila kundi la watu. Makundi
haya hutofautiana kulingana na umri kama vile watoto,
vijanabalehe na wazee. Vilevile, aina ya kazi wanazofanya
mwiliONLINE READING ONLY
kama vile watu wanaofanya kazi za nguvu nyingi na hali za
kiafya kama vile wagonjwa.
Watoto
Watoto ni kundi la watu waliopo katika kipindi cha ukuaji wa
kasi. Kwa kuwa wapo katika kipindi hicho muhimu wanahitaji
vyakula vya kujenga mwili kwa wingi. Vyakula hivyo ni kama vile
maziwa, nyama, samaki, maharage, njegere, kunde na mayai.
Vyakula hivyo husaidia kujenga mwili wa mtoto, kuimarisha
kinga ya mwili pamoja na ubongo. Vilevile, watoto wanahitaji
vyakula vya kuupa mwili nguvu. Vyakula hivyo huwawezesha
kupata nguvu za kucheza michezo mbalimbali na kufanya
shughuli wanazozimudu. Aidha, watoto wanahitaji vyakula vya
kulinda mwili ili kujenga kinga ya miili yao dhidi ya magonjwa.
Kielelezo namba 6 kinaonesha mlo kamili wa mtoto.
Vyakula
Vyakula vya kulinda
mwili
FOR
vya kujenga
Vyakula vya
kuupa mwili
nguvu
Kielelezo namba 6: Mlo kamili wa mtoto
6
14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 6
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 6 14/01/2025 18:38