Page 17 - SayansiStd4
P. 17
vyakula hivyo humsaidia mgonjwa kuimarisha misuli, mifupa
na kinga ya mwili.
Vilevile, mahitaji ya vyakula kwa wagonjwa hutofautiana
kulingana na aina ya ugonjwa. Hivyo, wagonjwa wanatakiwa
FOR ONLINE READING ONLY
kula mlo kamili kwa kuzingatia masharti na maelekezo ya
wataalamu wa afya. Kielelezo namba 10 kinaonesha mlo
kamili wa mgonjwa.
Vyakula vya
kuupa mwili
Vyakula vya nguvu
kulinda mwili
Vyakula vya
kujenga mwili
Kielelezo namba 10: Mlo kamili wa mgonjwa
Zoezi namba 1
1. Maria alikula wali na nyama siku ya Jumatatu. Je, huu ni
mlo kamili? Eleza sababu.
2. Pangilia mlo kamili kwa ajili ya mgonjwa kwa kutumia
vyakula vinavyopatikana nyumbani. Eleza sababu za
kujumuisha aina hizo za vyakula kwenye mlo huo.
3. Eleza tofauti ya mahitaji kati ya mlo wa mtoto na mtu
anayefanya kazi za kutumia nguvu nyingi.
10
14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 10 14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 10