Page 22 - SayansiStd4
P. 22
vizuri kwa kutumia pasi. Pasi huua vijidudu vya magonjwa na
hufanya nguo kuwa na mwonekano mzuri.
Usafi wa mazingira
FOR ONLINE READING ONLY
Mazingira machafu yanahatarisha usalama wa maisha ya
binadamu. Mazingira machafu ni chanzo cha mazalia ya
wadudu kama vile nzi na mbu. Wadudu hao hubeba vimelea vya
magonjwa mbalimbali. Vimelea hivyo husababisha magonjwa
kama vile kuharisha, kipindupindu, malaria na magonjwa ya
ngozi. Vilevile, hewa ikichafuka mtu huweza kupata magonjwa
ya mfumo wa hewa. Hivyo, uchafuzi wa mazingira husababisha
magonjwa mbalimbali ambayo hudhoofisha kinga ya mwili.
Inatupasa kusafisha mazingira mara kwa mara ili kuimarisha
afya na kinga ya mwili. Kielelezo namba 12 kinaonesha
wanafunzi wakifanya usafi wa mazingira.
Kielelezo namba 12: Wanafunzi wakifanya usafi wa mazingira
15
14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 15
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 15 14/01/2025 18:38