Page 23 - SayansiStd4
P. 23
Kazi ya kufanya namba 8
1. Tumia maktaba, matini mtandao na vyanzo vingine
FOR ONLINE READING ONLY
kutafuta taarifa kuhusu usafi wa nywele, kucha na nguo.
2. Fanya ukaguzi wa usafi wa nywele, kucha na nguo kwa
wanafunzi wenzako darasani, kisha utoe ushauri wa
kudumisha usafi.
Alama za usalama na taarifa muhimu katika mazingira
Katika mazingira tunayoishi, zipo alama au michoro
inayotuongoza kufanya mambo mbalimbali. Alama zinaweza
kuwasilishwa kwa maneno au picha. Alama hutoa maelekezo
yanayosaidia tuwe salama.
Kazi ya kufanya namba 9
Tembelea mazingira ya shule na ubainishe alama
zinazopatikana katika mazingira hayo.
Aina za alama
Alama za usalama zimegawanyika katika makundi makuu
manne. Makundi hayo ni alama za onyo au tahadhari, alama
za kuzuia au kukataza, alama za lazima au amri, na alama
za dharura. Kila aina ya alama za usalama huwasilishwa kwa
rangi na umbo maalumu. Rangi na maumbo ya alama hizi
huongozwa na taratibu za kiusalama za kimataifa.
Alama za onyo au tahadhari
Alama hizi zinatoa tahadhari ya tukio la hatari linaloweza
kutokea. Alama hizi zinaweza kuwekwa katika maeneo
16
14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 16
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 16 14/01/2025 18:38