Page 25 - SayansiStd4
P. 25
Alama za kuzuia au kukataza
Alama hizi zinatoa taarifa kuhusu jambo lisiloruhusiwa. Rangi
ya alama hizi ni nyekundu. Pia, zina umbo la duara, picha nyeusi
kwenye msingi mweupe na kingo nyekundu. Baadhi ya alama
FOR ONLINE READING ONLY
hizi zina mstari mwekundu wa kiegama. Mfano wa alama hizi ni
kama vile huruhusiwi kuingia na huruhusiwi kula wala kunywa.
Kielelezo namba 14 kinaonesha mifano ya alama za kuzuia au
kukataza.
Hairuhusiwi kula wala
Hairuhusiwi kuingia kunywa
Maji yasiyosalama Usitupe taka ovyo
Kielelezo namba 14: Mifano ya alama za kuzuia au kukataza
Alama za dharura
Alama hizi zinatoa maelekezo ya kufanya jambo husika
hususani dharura kama vile ajali. Alama hizo zinaonesha eneo
la karibu lenye usalama au maelekezo ya kufikia eneo salama
au vifaa vitakavyosaidia. Miongoni mwa alama hizo ni pamoja
na simu za dharura na sanduku la huduma ya kwanza. Alama
hizi zina rangi ya kijani. Pia, zina umbo la pembe nne, picha
18
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 18 14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 18