Page 29 - SayansiStd4
P. 29
muda wa bidhaa kuchotora, namna ya matumizi, viambata
vilivyotumika kutengeneza bidhaa na namna ya kuhifadhi.
Muda wa bidhaa kuchotora
FOR ONLINE READING ONLY
Ni muda ambao bidhaa husika inakwisha muda wake wa
matumizi. Bidhaa iliyochotora haifai kwa matumizi kwa sababu
huweza kuathiri afya. Muda wa kuchotora kwa bidhaa huandikwa
kwenye bidhaa kwa namna mbalimbali kati ya zifuatazo. Tarehe
ya kuchotora kwa lugha ya kiingereza huandikwa “Expiry
date” au kwa kifupi “ED, EXP au E.” . Hii inaonesha muda wa
kumalizika matumizi ya bidhaa husika. Hivyo, hutakiwi kutumia
baada ya muda huo. Kielelezo namba 17 kinaonesha mfano
wa taarifa ya kuchotora kwa bidhaa.
Kielelezo namba 17: Mfano wa taarifa ya kuchotora kwa bidhaa
Namna ya matumizi ya vitu
Kusoma na kuelewa maelekezo ya matumizi ya bidhaa kabla
ya kuanza kuitumia ni jambo la kuzingatia. Hii itasaidia uweze
kuitumia kwa usahihi na kulinda afya. Kwa mfano, bidhaa kama
vile dawa za kutibu magonjwa mbalimbali zinatakiwa kutumiwa
kwa kiwango sahihi ili kuepuka madhara ya kiafya. Kielelezo
namba 18 kinaonesha mfano wa maelezo ya kutumia dawa.
22
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 22 14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 22