Page 21 - SayansiStd4
P. 21
Baada ya kuoga, kausha mwili kwa taulo safi. Pia, paka mafuta
mwilini baada ya kuoga ili kuepuka ngozi kuwa kavu.
FOR ONLINE READING ONLY
Kazi ya kufanya namba 7
1. Tumia maktaba, matini mtandao au vyanzo vingine
kutafuta taarifa kuhusu vifaa na hatua za kuoga.
2. Wasilisha taarifa ulizozitafuta, darasani kwa ajili ya
majadiliano.
Usafi wa nywele
Nywele zinatunzwa kwa kuziosha mara kwa mara kwa kutumia
maji safi na sabuni. Vilevile, kwa kusuka, kunyoa au kuchana ili
zionekane safi na nadhifu. Nywele safi zinaepusha magonjwa
ya ngozi ya kichwa kama vile mapunye na wadudu kama vile
chawa.
Usafi wa kucha
Kucha za miguuni na mikononi zinatakiwa kuwa fupi ili kuepuka
uchafu. Kucha ndefu zinahifadhi uchafu unaoweza kuwa
na vimelea vya magonjwa. Tunapaswa kuosha mikono na
kusafisha kucha kwa maji safi na sabuni. Hii husaidia kuondoa
uchafu na vijidudu vinavyosababisha magonjwa.
Usafi wa nguo
Nguo zinatakiwa kufuliwa kwa maji safi na sabuni ili kuondoa
uchafu. Nguo chafu hufanya mwili kutoa harufu mbaya na
zinaweza kuleta magonjwa ya ngozi kamavile muwasho na
harara. Nguo iliyofuliwa inapaswa kukaushwa na kunyooshwa
14
14/01/2025 18:38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 14
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 14 14/01/2025 18:38