Page 141 - English_Form_3
P. 141

The Mbeya Regional Commissioner said later that the investor intended to
                establish another factory for starch. “The investor expects to purchase up
                to 40 tonnes of maize when production takes off,” he said.
          FOR ONLINE READING ONLY
                (b)  Translate the text: “The Sleeping Giants of Tanzania” into Kiswahili
                     using Artificial Intelligence (AI).
                (c)  Compare the two translations, the one you did manually and the one
                     you did with AI. Then, explain their differences and similarities.


           2.   Translate the following text into English.
                Maisha  ni  mtoto  wa kwanza  wa Bwana  na  Bibi  Chapakazi.  Maisha
                alisoma na kuhitimu Shahada ya Ualimu kutoka chuo kikuu maarufu hapa
                nchini.  Baada ya  kuhitimu  alipangiwa  kwenda  kufundisha  katika  shule
                moja iliyopo Kijiji cha Mwendakulima. Alipofika huko alishangaa watu
                wanavyoishi. Kulikuwa na nyumba zilizojengwa kwa miti, kuta za matope
                na kuezekwa kwa nyasi. Wakazi wa kjiji hicho hawakuwa na maji safi na
                salama. Mbaya zaidi, hapakuwa na umeme.  Maisha alitamani kukimbia na
                kurudi mjini au ikiwezekana kuacha kazi kabisa. Alikaa kwa muda kwenye
                jiwe lililokuwa karibu na shule. Baada ya kufikiri kwa muda aliona ile ni
                sehemu sahihi ya kuonesha uwezo wake.

                Alifika  ofisini  kwa  mkuu  wa  shule  na  kujitambulisha.  Mkuu  wa  shule
                alifurahi  sana maana  kwa sasa watakuwa  walimu watano.  Maisha
                alipangiwa vipindi na kuanza kufundisha kwa bidii. Kisha, aliwasiliana na
                mbunge wa jimbo hilo ambaye alifanya juhudi za kuleta maji na umeme
                kwenye shule na kijiji hicho. Hadi ninapoandika andiko hili, Maisha ana
                maisha mazuri, wakazi wa Kijiji hicho wana nyumba zilizojengwa kwa
                matofali ya kuchoma na kuezekwa kwa mabati. Vilevile kuna umeme na
                maji safi na salama. Kwa kweli Maisha amebadilisha maisha ya wananchi
                na wanafunzi. Kwa sasa shule hiyo ni miongoni mwa shule zinazofanya
                vizuri kwenye matokeo ya mitihani ya taifa ya Kidato cha Pili na cha Nne.
                Hakika uwezo wa mtu upo kwenye kubadili fikra na kutumia changamoto
                kama fursa ya mafanikio.













           English for Secondary Schools                              Student’s Book Form Three
                                                  134



                                                                                          17/09/2025   16:34:47
     ENGLISH F3 PB.indd   134
     ENGLISH F3 PB.indd   134                                                             17/09/2025   16:34:47
   136   137   138   139   140   141   142   143   144   145   146