Page 109 - Historia_Maadili
P. 109
Faharasa
Afrikanaizesheni Utaratibu wa kuwaingiza na kuwapa Waafrika wenye sifa
madaraka ya kiuchumi, kijamii na kisiasa baada ya nchi
za Kiafrika kupata uhuru kutoka kwa wakoloni
FOR ONLINE READING ONLY
Bepari Mtu ambaye ni mfanyabiashara na tajiri mkubwa
anayemiliki njia kuu za uzalishajimali kama vile viwanda
na masoko
Falsafa Stadi ya maarifa, imani, maisha, chanzo chake na sababu
za kuwapo kwake
Itikadi Imani au msimamo wa mtu au watu kuhusu jambo fulani
mfano dini, chama, mawazo
Kasumba Fikra za mtu zinazojengeka kutokana na kuathiriwa
kielimu, kiutamaduni au kiutawala na jamii fulani
iliyomzunguka
Kibaraka Mtu mwenye uwezo wa chini kifedha na anayetumiwa
na watu wengine kwa masilahi ya watu hao pasi na kujali
madhara wanayopata watu wengine
Propaganda Taarifa zisizo na ukweli ambazo hutumika katika
uhamasishaji wa watu ili wafuate mtazamo tofauti na ule
waliokuwa nao
Manamba Mfanyakazi aliyetoka mbali kwa ajili ya kufanya kazi
katika mashamba makubwa yaliyokuwa yanamilikiwa na
watu wengine hasa walowezi
Telegramu Taarifa ya maandishi inayotumwa kwa njia ya simu
Walowezi Watu wanaotoka nchi moja na kuhamia nchi au eneo
lingine kwa nia ya kudhibiti, kuendeleza, au kutumia
rasilimali za eneo hilo.
Wazawa Watu ambao wamezaliwa na kukulia katika eneo au nchi
fulani na ni wenyeji wa eneo hilo. Kwa mfano, “wazawa
wa Tanzania”
101
03/10/2024 18:15:21
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 101
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 101 03/10/2024 18:15:21

