Page 106 - Historia_Maadili
P. 106
Vilevile, Mapinduzi ya Zanzibar yalichochea muungano kati ya Zanzibar na
Tanganyika na hatimaye kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka
1964. Muungano huu uliwaleta pamoja watu kutoka asili na kanda mbalimbali.
Hivyo, kuimarisha hisia ya utambulisho wa kitaifa na umoja. Sababu za kihistoria
na kiuhusiano zilizosababisha kuungana kwa nchi hizi baada ya Mapinduzi zilifanya
muungano huu ufanikiwe na kuendelea kudumu hadi leo. Pia, nia ya viongozi wa
FOR ONLINE READING ONLY
pande zote mbili, yaani Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanganyika na
Sheikh Abeid Amani Karume wa Zanzibar, ya kudumisha umoja na mshikamano wa
kitaifa, hivyo ilichangia sana katika kufanikisha muungano huu.
Kujenga mshikamano
Mapinduzi ya Zanzibar yalichangia kwa kiasi kikubwa kuleta mshikamano wa
kitaifa miongoni mwa wananchi. Hii ilifanikishwa kupitia kuundwa kwa serikali
inayowakilisha makundi yote ya kijamii na kuondoa mgawanyiko wa kikabila na
kidini. Maadili ya mshikamano, upendo na umoja yalikuzwa na hivyo yameendelea
kuwa nguzo muhimu katika ujenzi wa taifa.
Aidha, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilipitisha kanuni za ujamaa na udugu ambazo
zilisisitiza usawa, umiliki wa pamoja wa rasilimali na mshikamano. Huduma za jamii
kama vile elimu, afya na makazi zilitolewa kwa usawa kwa wote bila kujali rangi,
kabila, au dini ya mtu. Misingi hii iliendana na ile ya serikali ya Tanganyika na itikadi
ya pamoja ilisaidia kuwaunganisha watu wa Zanzibar na Tanganyika chini ya dira
ya pamoja ya kitaifa.
Vilevile, Mapinduzi ya Zanzibar yalichochea hisia ya fahari ya kitaifa, uzalendo na
kujitolea kwa manufaa ya wote, ambayo yameendelea kujenga mfumo wa maadili
wa taifa hadi sasa. Mshikamano huu ulikuwa muhimu katika kuhamasisha wananchi
kuunga mkono serikali mpya na sera zake. Serikali ya ASP ilifanya kazi ya kukuza
mshikamano wa kijamii kwa kuzuia sera zote za kibaguzi na kuweka misingi thabiti
ya usawa, utu, heshima na kuboresha hali ya maisha ya watu katika nyanja zote.
Kazi ya kufanya 6.3
Soma matini mbalimbali yanayohusu mapinduzi ya kisiasa katika nchi mbalimbali
duniani, kisha eleza ni kwa namna gani mapinduzi yanavyoweza kujenga umoja
na mshikamano kwa taifa linalohusika.
98
03/10/2024 18:15:20
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 98 03/10/2024 18:15:20
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 98

