Page 104 - Historia_Maadili
P. 104
Zoezi la 6.3
1. Eleza nafasi ya ASP katika kufanikisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
2. Eleza ni kwa namna gani huduma za kijamii kama vile elimu, afya na makazi
FOR ONLINE READING ONLY
zilitolewa kulingana na matabaka ya rangi Zanzibar.
3. Ni kwa namna gani ubaguzi wa rangi ulichochea Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar?
Kazi ya kufanya 6.2
Soma matini mbalimbali kupitia mtandao yanayohusu Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar, kisha andika maelezo kwa ufupi kuhusu:
(a) Namna Mapinduzi yalivyofanyika;
(b) Viongozi walioongoza Mapinduzi; na
(c) Ulichojifunza kutokana na Mapinduzi hayo.
Mchango wa Mapinduzi wa Matukufu ya Zanzibar
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 yalileta mabadiliko makubwa
katika historia ya Zanzibar na yalikuwa na athari kubwa katika ukanda wa Afrika
Mashariki na maeneo mengine. Mapinduzi hayo yalisababisha kuondolewa kwa
utawala wa kisultani na kuanzishwa kwa serikali iliyoongozwa na wazalendo wa
Chama cha Afro-Shirazi (ASP). Chama cha ASP kiliongoza kwa misingi ya utu, haki
na ustawi wa watu wote bila kuzingatia tofauti za asili, hadhi au kabila. Mchango
wa Mapinduzi hayo unajidhihirisha katika nyanja mbalimbali kama vile kujenga
umoja, kuimarisha mshikamano na kuendeleza maadili katika jamii za Kizanzibari
na Tanzania kwa ujumla.
Kujenga umoja
Mapinduzi yalisaidia kuvunja migawanyiko na chuki zilizojengwa kutokana na hali
ya ubaguzi katika jamii wakati wa ukoloni. Kwa kuwapindua watawala waliokuwa
wakionekana kama wawakilishi wa wakoloni walioondoka, Mapinduzi yalileta umoja
96
03/10/2024 18:15:20
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 96
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 96 03/10/2024 18:15:20

