Page 99 - Historia_Maadili
P. 99
Mapinduzi ya Zanzibar yalitokana na sababu nyingi za kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Kwa mfano, Waarabu, ambao walikuwa wachache, walipewa upendeleo na walitawala
kisiasa na kiuchumi. Hali hii haikuwaridhisha Waafrika waliokuwa wengi. Waarabu
walihodhi madaraka, ardhi na utajiri mwingine wa Zanzibar, huku Waafrika wakiwa
wafanyakazi wa watawala.
FOR ONLINE READING ONLY
Aidha, jamii ya Zanzibar iliathiriwa kwa kiasi kikubwa na mchanganyiko mkubwa
wa watu wenye tamaduni tofauti. Kulikuwa na watu wenye tamaduni za Waarabu,
Waafrika na Wahindi. Hivyo, jamii iligawanyika katika makundi ya watu kulingana
na rangi na asili ya jamii iliyohusika. Kwa mfano, jumuiya za Waarabu, hususani
Waarabu wa Oman, walikuwa na nguvu kubwa za kisiasa na kiuchumi na walikuwa na
hadhi ya juu zaidi. Wahindi walikuwa na nguvu za kiuchumi kwa kushikilia biashara
nyingi, hivyo walikuwa ni kundi lenye hadhi ya kati. Wakati huo huo, Waafrika
waliokuwa wengi na walikuwa na hadhi ya chini kabisa katika jamii, wakiwa
hawana nguvu za utawala wala uchumi. Utaratibu huu uliathiri kanuni za kimaadili
na kijamii za wakati huo, kwani heshima, utu na tabia ziliamuliwa kutokana na asili
(rangi), hadhi na nafasi ya mtu katika jamii.
Kutokana na kukosa haki zao za msingi, vyama vya siasa vya ASP, ZNP na ZPPP
viliongeza shinikizo kwa serikali ya kikoloni kuwapatia uhuru Wazanzibari. Vuguvugu
hili halikuwa rahisi na lilichukua sura na mitazamo tofauti. Hata hivyo, baada ya
malumbano makali na chaguzi nyingi kufanyika, Uingereza iliutoa uhuru kwa Zanzibar
tarehe 10 Desemba 1963. Uhuru huu ulikuwa wa serikali ya mseto wa vyama vya
ZNP na ZPPP. Katika kipindi hiki, Waziri Mkuu alikuwa Mohammed Shamte, huku
Sultani Jamshid bin Abdullah Al Said akibaki kwenye nafasi yake kama kiongozi wa
nchi. Uhuru huu haukuungwa mkono na wengi, hasa Waafrika, ambao waliona kuwa
Waingereza wamekabidhi serikali kwa Waarabu badala ya wananchi wote.
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalikuwa ni kilele cha harakati za mapambano
ya ukombozi wa Wazanzibari. Mapambano haya yalikuwa ni matokeo ya uchaguzi
na uhuru uliotolewa tarehe 10 Desemba 1963 chini ya serikali ya Waziri Mkuu
Mohammed Shamte na Sultani Jamshid bin Abdullah Al Said, uhuru ambao
ulijulikana kama “uhuru wa wachache.” Hivyo, kufikia tarehe 12 Januari 1964,
91
03/10/2024 18:15:19
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 91
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 91 03/10/2024 18:15:19

