Page 102 - Historia_Maadili
P. 102
Mathalani, uchaguzi wa Julai 1963 uliwapa ushindi muungano wa ZNP na ZPPP
ambao walipata viti 18 dhidi ya viti 13 vya ASP. Mohamed Shamte wa ZPPP akawa
Waziri Mkuu wa kwanza wa Zanzibar, jambo ambalo lilionekana kuwa ni la upendeleo
na kuuendeleza ubaguzi. Wazanzibari walichoka kutawaliwa na wageni kwa muda
mrefu na walihitaji kujitawala wenyewe. Hivyo basi, Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
yalikuwa ni hatua muhimu ya kujikomboa na kuupata uhuru ili kujenga maendeleo,
FOR ONLINE READING ONLY
kulinda utamaduni na maadili ya watu wa Zanzibar.
Sababu za kijamii: Kabla ya kuja kwa utawala wa Waarabu, utamaduni wa jadi wa
jamii za Kizanzibari ulikuwa na tabia na sifa maalumu zinazotokana na mazingira,
mila na desturi za jamii hizo. Wazanzibari walifundishwa kuheshimu watu wa rika
zote, wakiwemo wazazi, wazee na viongozi wa mila. Aidha, watoto walilelewa kwa
kushiriki katika kazi za kijamii kama kilimo na uvuvi. Pia, kulikuwa na mgawanyo
wa majukumu katika familia na jamii. Kwa mfano, wanawake walijihusisha na
shughuli za ususi wa vikapu na mikeka kwa kutumia majani mbalimbali kama ya
ukindu, minazi na miti ya porini. Wanaume walijihusisha na uvuvi, uwindaji, kilimo,
pamoja na ufundi wa kutengeneza zana za kilimo na uvuvi. Pia wanaume walijenga
nyumba za jadi kwa kutumia udongo, makuti, mawe na miti hasa mikoko.
Vilevile, jamii iliishi kwa kuzingatia misingi ya umoja, haki na amani. Matukio kama
vile harusi, tohara na mazishi yalitumika kuwaunganisha watu pamoja. Vyombo vya
muziki kama ngoma, njuga, filimbi na marimba vilikuwa maarufu katika kuenzi
maadili na utamaduni wa Wazanzibari. Muziki na ngoma za jadi zilitumika katika
sherehe na matukio haya muhimu ya kijamii kama vile unyago kwa wasichana na
jando kwa wavulana. Hivyo, maadili haya na utamaduni wa jadi vilijenga msingi wa
jamii ya Wazanzibari kabla ya kuja kwa wageni ambao walileta athari za kiutamaduni,
kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Kuja kwa ukoloni kulileta ubaguzi katika jamii. Watu walianza kuheshimiwa kutokana
na vyeo na asili yao (rangi). Maadili ya kuheshimu watu wa rika na tabaka zote
hayakuzingatiwa. Vilevile, huduma za jamii kama vile maji, umeme na makazi
zilitolewa kwa ubaguzi. Wazanzibari walibaguliwa katika nyanja za elimu, afya,
makazi na umiliki wa rasilimali kama vile ardhi. Kwa mfano, mwaka 1955, asilimia
14 ya bajeti ya Serikali katika elimu ilielekezwa kwenye shule za Wahindi, wakati
kipindi hicho Wahindi walikuwa 6% tu ya watu wote wa Zanzibar. Huduma muhimu
za kijamii, kama vile maji safi, umeme na makazi, ziliimarishwa katika Mji Mkongwe
ambako tabaka la Waarabu, Wahindi, pamoja na familia za wakoloni au Wazungu
ziliishi. Huduma hizi hazikupatikana maeneo mengine kama Ng’ambo ambako
Waafrika wengi waliishi.
94
03/10/2024 18:15:19
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 94 03/10/2024 18:15:19
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 94

