Page 101 - Historia_Maadili
P. 101
12 Januari 1964, Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar yalifanyika. Sultani Jamshid bin
Abdullah Al Said aling’olewa madarakani
pamoja na serikali yake chini ya Waziri
Mkuu Mohamed Shamte wa ZPPP.
FOR ONLINE READING ONLY
Hatimaye tarehe 12 Januari 1964, Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya ASP
ikatangazwa. Kielelezo 6.2 kinaonesha
baadhi ya viongozi walioshiriki katika
Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964. Kielelezo 6.2: Baadhi ya viongozi walioshiriki
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mwaka 1964
Kulikuwa na sababu kadhaa zilizosababisha Mapinduzi ya Zanzibar. Sababu hizi
zilichochewa na madai ya muda mrefu dhidi ya utawala wa sultani, ambaye alionekana
kuwa mwakilishi wa Waingereza. Baadhi ya sababu hizo ni kama zifuatazo:
Sababu za kisiasa: Kabla ya ujio wa Waarabu, Zanzibar ilikuwa imegawanyika
katika maeneo mbalimbali ya kiutawala na kila eneo lilikuwa na kiongozi wake.
Baadaye, watawala wa kienyeji kama vile Mwinyi Mkuu kwa upande wa Unguja
na Makamandume kwa Pemba, waliunganisha mamlaka ndogondogo na kuunda
himaya kubwa zaidi. Viongozi hawa walizisimamia sheria na taratibu za kijamii na
waliheshimiwa sana. Walikuwa na jukumu la kuamua migogoro, kuongoza sherehe za
kijamii na kusimamia maadili katika jamii walizoziongoza. Hata hivyo, hali ilibadilika
baada ya kuja kwa utawala wa wageni, hasa kuanzia kipindi cha Usultani wa Waarabu.
Watawala wa kienyeji waliondolewa na katika utawala huu, kuanzia wakati wa
usultani hadi ukoloni wa Waingereza, masilahi ya wenyeji hayakuzingatiwa wala
hayakupewa kipaumbele. Kwa mfano, wenyeji hawakushirikishwa kwenye vyombo
vya kutoa uamuzi na kuwa viongozi serikalini.
Hata hivyo, kulikuwa na mabadiliko kidogo baada ya kuundwa kwa Baraza la Kutunga
Sheria mwaka 1925. Wakati huu Waafrika wachache walipata nafasi, ingawa idadi
kubwa ya wajumbe ilikuwa ni Waarabu na Wahindi. Wazanzibari hawakupata uhuru wa
kujitawala na kufanya uamuzi wao wenyewe. Wajumbe hawa wachache hawakuweza
kutetea masilahi ya Waafrika walio wengi Zanzibar. Hata uhuru uliopatikana baada
ya uchaguzi wa mwaka 1963 ulikuwa ni mwendelezo wa mizizi ya ukoloni ya
kutowatendea haki na heshima Wazanzibari.
Vilevile, chaguzi zote tatu zilitawaliwa na mizengwe iliyosababisha kukataliwa kwa
matokeo. Chaguzi zilifuatiwa na fujo na ulaghai na ushindi wa ASP haukutambuliwa.
93
03/10/2024 18:15:19
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 93 03/10/2024 18:15:19
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 93

