Page 97 - Historia_Maadili
P. 97
Sura ya Sita Mapinduzi Matukufu
ya Zanzibar
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Katika harakati za kudai uhuru, njia mbalimbali zilitumika. Njia hizo zilijumuisha
matumizi ya mtutu wa bunduki, mapinduzi na njia ya amani au katiba. Zanzibar
ilitumia njia ya mapinduzi katika harakati za kudai uhuru wa kweli. Katika sura
hii, utajifunza kuhusu dhana ya mapinduzi, chimbuko la Mapinduzi Matukufu
ya Zanzibar, sababu zake na mchango wake katika kujenga umoja, mshikamano
na maadili ya taifa. Umahiri utakaoujenga utakuwezesha kuyatetea, kuyalinda
na kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Fikiri
Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Dhana ya mapinduzi
Neno ‘mapinduzi’ linaweza kuwa na maana nyingi kulingana na mazingira tofauti.
Hata hivyo, katika muktadha huu, mapinduzi yanarejelea harakati za kubadili utawala
wa kisiasa ndani ya muda mfupi, kwa kutumia nguvu za kijeshi au nguvu za umma.
Kuna aina mbili za mapinduzi, ambazo ni mapinduzi ya kisiasa na mapinduzi ya
kijeshi.
Mapinduzi ya kisiasa ni yale yanayofanywa kupitia nguvu za umma. Katika mapinduzi
haya, wananchi walio wengi na wanyonge huwaondoa watawala wachache kwa
kuzitumia nguvu za umma, mara nyingi bila kumwaga damu kwa kiasi kikubwa.
Ili kufanikisha jambo hili, wananchi wanaweza kuandamana au kuzitumia mbinu
nyingine za kijamii.
89
03/10/2024 18:15:19
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 89 03/10/2024 18:15:19
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 89

