Page 94 - Historia_Maadili
P. 94
Kazi ya kufanya 5.5
Tafuta taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo mtandao na andika maelezo
zaidi kuhusu uanzishwaji wa mfumo wa chama kimoja cha siasa na mchango
FOR ONLINE READING ONLY
wake katika ujenzi wa taifa.
Zoezi la 5.4
1. Eleza mchango wa mfumo wa chama kimoja katika ujenzi wa taifa katika
kipindi cha 1961 hadi 1966.
2. Ni kwa namna gani tatizo la ardhi Zanzibar lilitatuliwa mara baada ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar?
3. Fafanua mchango wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika kukuza maadili na
uzalendo kwa vijana mara baada ya uhuru.
4. Toa sababu tano zilizosababisha serikali kuvunja mamlaka za jadi mwaka
1962.
Changamoto za ujenzi wa taifa
Kipindi cha mwaka 1961 hadi 1966 Taifa lilipitia changamoto mbalimbali za kiuchumi.
kijamii na kisiasa. Kwa mfano, sekta ya kilimo ilipitia changamoto mbalimbali
ikiwemo matumizi ya zana duni. Pia, kulikuwa na ukosefu wa wataalamu wa kilimo na
uhaba wa masoko ya uhakika ya bidhaa. Hata hivyo, viwanda vilikuwa havijaimarika
kutokana na upungufu wa wataalamu wa kuviendesha na pia kulikuwa na uhaba wa
vipuri. Matatizo ya kifedha na mitaji yaliathiri juhudi za awali za kuleta maendeleo
nchini. Aidha, kukosekana kwa uhusiano wa moja kwa moja kati ya kilimo na
viwanda kuliathiri maendeleo ya sekta zote mbili. Hata hivyo, pamoja na changamoto
hizi zote, pato la taifa liliendelea kukua na kuimarika na hili liliendelea kuipa Tanzania
heshima kimataifa. Kwa ujumla, kulikuwa na changamoto kadhaa zilizoathiri ujenzi
wa taifa mara baada ya uhuru.
Uasi wa jeshi mwaka 1964: Uasi wa Januari 20-27, 1964, pale Colito (sasa Lugalo),
ambapo kikundi kidogo cha wanajeshi wa Tanganyika Rifles (TR) kiliasi na kutaka
kuipindua serikali. Jaribio hilo lilizimwa na waliohusika walipewa adhabu kali, kama
kufukuzwa jeshini, kufungwa na kuwekwa kizuizini kwa muda mrefu. Uasi huu
ulisababisha kuundwa kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
86
03/10/2024 18:15:19
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 86
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 86 03/10/2024 18:15:19

