Page 89 - Historia_Maadili
P. 89
Huduma za jamii
Mabadiliko katika utoaji huduma za jamii yalilenga kubadilisha mfumo wa kikoloni na
kuunda mfumo unaokidhi mahitaji ya taifa huru. Mfumo mpya wa utoaji huduma za
jamii ulilenga kujenga jamii yenye ujuzi, maarifa na afya katika ujenzi wa taifa huru.
Mara baada ya uhuru vipaumbele vya elimu vilibadilika kuendana na matakwa ya
FOR ONLINE READING ONLY
nchi. Baada ya uhuru, wataalamu wengi Wazungu waliondoka, hivyo watumishi
Waafrika walibaki wachache. Hii ilileta umuhimu wa kuwaandaa wataalamu wazawa.
Kwa maana hiyo, serikali ilijikita kutoa elimu kwa wote iliyokuwa na lengo la kufanya
kila raia anakuwa na ufanisi katika kazi zake za kila siku na inayoweza msaidia
kujiendeleza zaidi kielimu. Hii ilitekelezwa zaidi upande wa elimu ya msingi ambapo
shule mpya zilijengwa na kuongeza idadi ya wanafunzi. Pia, Mpango wa Kwanza wa
Miaka Mitano ulijikita katika upanuzi wa elimu ya sekondari ili kuandaa wataalamu
na viongozi wa baadaye, ingawa changamoto za rasilimali na walimu zilikuwepo.
Pamoja na hayo, elimu hii ilitolewa kwa watu wote bila kujali jinsia, ukanda, hadhi
au kabila tofauti na elimu ya kikoloni. Serikali ilianzisha na kujenga shule mpya na
kuongeza idadi ya wanafunzi waliojiunga na elimu ya sekondari.
Vilevile, serikali ilianzisha vyuo vya ufundi ili kutoa mafunzo ya ufundi na ufundi
stadi kwa vijana, jambo ambalo lilikuwa muhimu kwa kuimarisha sekta ya viwanda
na kilimo. Kwa mfano, Chuo cha Ufundi Dar es Salaam, ambacho kilipanuliwa mwaka
1962 na kuanza kutoa elimu ya ufundi mwaka 1964. Aidha vyuo vya ualimu vilianzishwa
na kupanuliwa. Baadhi ya vyuo hivyo ni Chuo cha Ualimu Morogoro (Kigurunyembe)
ambacho hapo mwanzo kilimilikiwa na Wamisionari. Chuo hiki kilijikita katika kuandaa
walimu wa kwenda kufundisha shule za msingi ili kuendana na upanuzi wa shule za msingi
nchini walipoanzisha Daraja la IIIA mwaka 1961 na Diploma (stashahada) baadae mwaka
1970 baada ya kupandishwa hadhi na kuanza kutoa mafunzo ya Diploma (stashahada)
mwaka 1966.
Maendeleo katika sekta ya elimu hayakuishia katika kada za chini na kati tu, bali
yalienda hadi katika elimu ya juu. Kwa mfano, mwaka 1961 serikali ilikianzisha
Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (University College of Dar es Salaam) chini
ya Chuo Kikuu cha London. Hii ilikuwa hatua muhimu katika kuandaa wasomi na
wataalamu mbalimbali wa ngazi ya juu.
Upanuzi wa miundombinu ya afya, ikijumuisha ujenzi wa zahanati na hospitali za
umma vijijini na mijini. Upanuzi mkubwa ulikuwa ni ule wa Hospitali ya Muhimbili
mnamo mwaka 1961 mara baada ya uhuru. Upanuzi huu ulisababisha kubadili jina
toka Hospitali ya Princess Margareth na kuwa Hospitali ya Muhimbili. Hii ilikuwa
hatua kubwa sana katika sekta ya afya. Pia, serikali ilijenga na kupanua hospitali za
kikanda na pia kujenga vituo vya afya na zahanati katika maeneo ya mijini na vijijini.
Lengo lilikuwa kufikisha huduma kwa wananchi wengi, hususani wale wa maeneo ya
vijijini ambao awali walikuwa hawapati huduma bora za afya. Juhudi hizi zilihusisha
kuajiri na kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya.
81
03/10/2024 18:15:18
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 81 03/10/2024 18:15:18
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 81

