Page 87 - Historia_Maadili
P. 87
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Tarehe 26 Aprili, 1964, ni tukio muhimu
la kihistoria na kisiasa katika kipindi hicho. Muungano huu ulitokana na uhusiano
wa kihistoria uliokuwepo kati ya jamii za Tanganyika na Zanzibar, uhusiano ambao
ulitokana kwa kiasi kikubwa na udugu, historia na biashara uliojengwa karne nyingi
kabla ya ukoloni. Aidha, Muungano huu ulikuwa nguzo muhimu katika kulinda
uhuru na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Muungano huu uliunda utaifa mpya wa
FOR ONLINE READING ONLY
Utanzania.
Uanzishwaji wa mfumo wa chama kimoja cha kisiasa mwaka 1965: Tanzania iliamua
kufuta mfumo wa vyama vingi na kuanzisha mfumo wa chama kimoja. Vyama
vilivyoruhusiwa kufanya siasa vilikuwa ni TANU kwa Tanganyika na ASP kwa
upande wa Zanzibar. Sababu ya kuanzisha mfumo wa chama kimoja ilikuwa ni kuleta
maendeleo na kuudumisha umoja na mshikamano. Uanzishwaji wa mfumo huu
ulienda sambamba na uanzishwaji wa siasa ya ujamaa na kujitegemea mwaka 1967.
Zoezi la 5.1
1. Pendekeza mikakati ya kuboresha mfumo wa ubalozi wa nyumba kumi
katika kuimarisha ulinzi na usalama kwenye mazingira unayoishi.
2. Kwa nini sera ya Afrikanaizesheni ilikuwa muhimu mara baada ya uhuru wa
Tanganyika na Mapinduzi ya Zanzibar?
3. Eleza umuhimu wa kuwa na vijana wenye uzalendo katika taifa.
4. Eleza umuhimu wa Jeshi la Kujenga Taifa katika kujenga maadili ya vijana
wa Kitanzania.
Uchumi na huduma za jamii
Mara baada ya uhuru, serikali iliweka mkazo katika kujenga mifumo imara ya uchumi
na huduma za jamii. Harakati za kujenga mifumo hii ziliongozwa na nadharia ya
kupambana na maadui watatu: ujinga, maradhi na umasikini. Kuwapo kwa ujinga,
maradhi na umasikini kulisababishwa na mifumo ya kiuchumi na kijamii iliyojengwa
wakati wa ukoloni. Hivyo, katika kipindi hiki, kulikuwa na umuhimu wa kujenga na
kuimarisha uchumi na huduma za jamii.
Uchumi
Mara baada ya uhuru, Tanganyika na Zanzibar zilirithi mfumo wa uchumi wa kikoloni
ambao ulinufaisha watu wachache, wengi wao wakiwa wageni. Uchumi huu haukuwa
na uwiano wa maendeleo; kulikuwa na maendeleo hafifu katika sekta ya kibiashara,
huku sekta ya viwanda ikiwa ndogo na kumilikiwa na wageni. Kulihitajika kujenga
79
03/10/2024 18:15:17
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 79
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 79 03/10/2024 18:15:17

