Page 82 - Historia_Maadili
P. 82
Kazi ya kufanya 4.5
Tafuta taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo mitandao, kisha bainisha jinsi
maadili mengine ya Kitanzania yaliyotunzwa wakati wa harakati za kudai uhuru
wa Tanganyika na Zanzibar.
FOR ONLINE READING ONLY
Zoezi la 4.4
1. Eleza jinsi maadili ya kikoloni yalivyoathiri maadili ya jamii za Kitanzania
wakati wa ukoloni.
2. Kwa kurejea muktadha wa kipindi cha kupigania uhuru wa Tanganyika na
Zanzibar. Fafanua misingi ya usemi kuwa, “umoja ni nguvu, utengano ni
udhaifu”.
3. Pendekeza mikakati ya kudumisha maadili yaliyotunzwa wakati wa harakati
za kudai uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
4. Eleza mikakati ya kujenga uzalendo kwa vijana katika mazingira ya sasa.
Zoezi la marudio
1. Je, unafikiri ni kwa nini harakati za kudai uhuru wa Tanganyika na Zanzibar
zilifanikiwa kuwaunganisha wananchi?
2. Kwa nini vyama vya TANU na ASP vilipata uungwaji mkono mkubwa
ukivilinganisha na vyama vingine vya siasa wakati wa kupigania uhuru?
3. Eleza mchango wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid
Amani Karume katika kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
4. Eleza kwa nini uhuru wa Tanganyika na Zanzibar unapaswa kulindwa.
5. Fafanua maadili yaliyodumishwa wakati wa harakati za kudai uhuru wa
Tanganyika na Zanzibar.
6. Kwa kutumia mifano, eleza maana ya uzalendo.
7. Jadili mchango wa viongozi wa kisiasa wa sasa katika kutunza maadili na
kujenga uzalendo.
74
03/10/2024 18:15:17
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 74
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 74 03/10/2024 18:15:17

