Page 77 - Historia_Maadili
P. 77
Zoezi la 4.3
1. Unafikiri ni kwa nini serikali za kikoloni ziliwazuia Waafrika kuanzisha
vyama vya kisiasa?
2. Je, unafikiri ni kwa nini vyama vya kiraia vilivyoanzishwa wakati wa
FOR ONLINE READING ONLY
harakati za kudai uhuru vilibadilika na kuanza kujihusisha na siasa?
3. Eleza mchango wa vyama vya siasa katika harakati za kudai uhuru wa
Tanganyika na Zanzibar.
4. Fafanua mafanikio na changamoto zinazokabili vyama vya siasa kwa sasa.
5. Eleza wajibu wa vyama vya siasa katika kuikuza demokrasia nchini.
Mchango wa harakati za kupinga uvamizi na ukoloni
Mchango wa harakati za kupinga uvamizi na ukoloni ulikuwa ni pamoja na kutunza
maadili na kujenga uzalendo.
Kutunza maadili
Ujenzi wa maadili ni mchakato wa kihistoria kwa kuwa unatokana na hisia ambazo
watu au jamii wamezikuza kwa miaka mingi kama sehemu ya harakati zao za kuleta
maendeleo na uhuru katika jamii au nchi yao. Maadili ni muhimu kutunzwa kwa
kuwa yanaleta fahari, umoja, ujasiri na mienendo inayokubalika katika jamii. Hivyo,
harakati za kupinga ukoloni nazo zilichangia katika utunzaji wa utambulisho wa
Mtanzania, ambao ni pamoja na umoja, utu, mshikamano na lugha ya Kiswahili.
Umoja
Harakati za kupinga uvamizi na mifumo ya kikoloni zilichangia pia katika kudumisha
maadili ya umoja miongoni mwa jamii za Kitanzania. Kabla ya ukoloni, jamii za
Kitanzania zilikuwa zimegawanyika katika makabila mbalimbali. Kila kabila lilikuwa
na utaratibu wake wa maisha, ikiwa ni pamoja na mila na desturi zake. Pia, inapaswa
kukumbukwa kuwa wakoloni walikuwa na nguvu kubwa za kijeshi na walimiliki
silaha bora zaidi ikilinganishwa na silaha za jadi zilizotumiwa na jamii za Kitanzania
wakati huo. Hivyo, viongozi wa jamii mbalimbali za Kitanzania walihimiza umoja
miongoni mwa wanajamii ili kuwa na nguvu ya kukabiliana na uvamizi na utawala
wa kikoloni. Waliamini kuwa “umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.”
Aidha, kuelekea kipindi cha kupata uhuru, kwa mfano, viongozi kama Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere, Sheikh Abeid Karume na wengineo waliunganisha makabila
na jamii mbalimbali. Hali hii, ilisaidia kuendeleza mapambano ya ukombozi kwa
pamoja kama jamii moja ya Watanganyika na jamii ya Wazanzibari katika kudumisha
69
03/10/2024 18:15:16
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 69
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 69 03/10/2024 18:15:16

