Page 76 - Historia_Maadili
P. 76

Chama cha ASP kilikuwa na malengo mengi, yakiwemo kupigania uhuru wa Zanzibar,
          kuunda serikali ya kidemokrasia katika visiwa vya Unguja na Pemba, kuondoa ubaguzi
          wa aina yoyote katika visiwa hivyo, kudumisha uhuru wa Zanzibar na watu wake,
          pamoja na kuwaandaa wananchi wawe tayari kupigania uhuru wao.

          Vyama vya siasa, hasa TANU kwa Tanganyika na ASP kwa Zanzibar, vilikuwa na
        FOR ONLINE READING ONLY
          mchango muhimu katika kukuza harakati za kupigania uhuru wa nchi hizo. Kwa
          namna moja ama nyingine, vyama hivi viliunganisha wananchi na kuwaongoza
          katika mapambano ya kuudai uhuru. Vilihamasisha wananchi kujiunga navyo na
          kushiriki katika harakati za kuudai uhuru wa nchi zao. Viongozi wa TANU na ASP
          walitangaza falsafa na sera za vyama hivyo kwa wanachama na wananchi wote kwa
          ujumla. Pia, vyama hivi viliandaa mikutano ya kisiasa na kuhamasisha wanachama
          pamoja na wananchi kuhudhuria mikutano hiyo.

          Aidha, vyama vya siasa vilianzisha matawi katika maeneo mbalimbali ya nchi ili
          kuvutia wanachama wengi zaidi. Vyama hivi vilitoa elimu na mafunzo ya kiuongozi
          na kisiasa kwa viongozi wa matawi na ngazi ya kitaifa. Katika chaguzi mbalimbali
          zilizofanyika kabla ya uhuru, vyama vya siasa vilishiriki na baadhi ya vyama
          vilifanikiwa kupata wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria. Ni muhimu pia
          kufahamu kuwa, vyama kadhaa, hasa TANU na ASP, vilianzisha vyombo vya habari
          ili kuendeleza harakati za kudai uhuru. Kwa mfano, TANU kilianzisha gazeti lililoitwa
          ‘Sauti ya TANU’ na ASP kilianzisha
          ‘Sauti  ya  ASP.’ Hivyo basi, ni
          dhahiri kuwa vyama vya siasa
          vilichochea kukua kwa harakati za
          kudai  uhuru wa  Tanganyika na
          Zanzibar. Hata hivyo, vyama hivyo
          vilikabiliana na changamoto nyingi,
          ikiwemo upinzani mkali kutoka kwa
          serikali ya kikoloni. Kielelezo 4.7
          kinaonyesha picha ya Mwalimu
          Nyerere akiwa na mawakili wake
          wakielekea mahakamani kujibu kesi      Kielelezo 4.7: Mwalimu Nyerere akiwa na
          ya uchochezi.                              mawakili wakielekea mahakamani



           Kazi ya kufanya 4.4


            Tafuta taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo mtandao na bainisha mbinu
            nyingine zilizotumika katika harakati za kuudai uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.






                                                  68




                                                                                        03/10/2024   18:15:16
   HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd   68                                         03/10/2024   18:15:16
   HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd   68
   71   72   73   74   75   76   77   78   79   80   81