Page 80 - Historia_Maadili
P. 80
wa Kijerumani na baadaye wa Kiingereza. Baadhi ya Watanzania waliochangia katika
ujenzi wa uzalendo kwa jamii zao ni pamoja na Abushiri bin Salim al-Harthi wa
Pangani, Mangi Meli wa Old Moshi, Mtemi Isike wa Unyanyembe, Mtwa Mkwawa
wa Iringa, Mwene Machemba wa Wayao, Nkosi Songea, Mbano wa Wangoni na Liti
Kidanka wa Singida.
FOR ONLINE READING ONLY
Hivyo, harakati za wazalendo hawa kupinga uvamizi wa kikoloni, ulichangia katika
ujenzi wa maadili ya uzalendo kwani wananchi walijitoa kushiriki katika vita na
ulinzi wa jamii zao. Wanajamii walichangia ujenzi wa uzalendo pale walipopinga
waziwazi sera za wakoloni na walipojitoa kushiriki katika vita dhidi ya wavamizi.
Harakati za kupinga utawala na mifumo ya kikoloni zilipanda mbegu ya uzalendo
kwa jamii za Kitanzania, kupenda jamii zao na hata kujitoa maisha yao kupambana
dhidi ya uvamizi wa kikoloni. Hali hii ilichangia katika ujenzi wa kizalendo ndani
ya jamii zao na baadaye kwa nchi nzima ya Tanzania.
Vilevile, harakati za kudai uhuru wa Tanganyika na Zanzibar nazo zilichangia katika
ujenzi wa uzalendo miongoni mwa Watanzania. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
na Sheikh Abeid Amani Karume pia walitoa mchango mkubwa nyakati zote za harakati
za kudai uhuru. Walijitolea sehemu kubwa ya maisha yao kupigania uhuru wa
Tanganyika na Zanzibar. Mwalimu Nyerere kwa upande wa Tanganyika alitoa
mchango mkubwa katika kubadili TAA na kuanzishwa kwa TANU tarehe 7 Julai
1954, kwani chama cha TAA kilikuwa na mwelekeo wa kijamii zaidi kuliko siasa.
Pia, Mwalimu Nyerere akiwa
mwenyekiti wa TANU na Sheikh
Karume akiwa mwenyekiti wa ASP
walifanikiwa kuwaunganisha
viongozi na wananchi hadi kupatikana
kwa uhuru wa Tanganyika na Zanzibar
mtawalia. Kielelezo 4.8 kinaonesha
picha ya viongozi wakuu wa TANU
na ASP, Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere na Sheikh Abeid Amani Kielelezo 4.8: Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Karume. na Sheikh Abeid Amani Karume
Aidha, viongozi wa vyama vya TANU na ASP pamoja na viongozi wengine katika
ngazi mbalimbali walikuwa wazalendo, kwani walitoa mchango muhimu katika
kuanzisha na kuendeleza harakati za kudai uhuru. Uzalendo wao ulidhihirika kupitia
72
03/10/2024 18:15:16
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 72 03/10/2024 18:15:16
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 72

