Page 75 - Historia_Maadili
P. 75
Vyama vya siasa
Umoja wa Waafrika ulioitwa African Association (AA) uliundwa mwaka 1929 na
mnamo mwaka 1948 ulipewa jina jipya la Tanganyika African Association (TAA).
Mwaka 1954, chama hiki kilibadilishwa jina tena na kuwa chama rasmi cha siasa
kwa jina la TANU.
FOR ONLINE READING ONLY
Chama cha TANU kilikuwa na malengo mengi na baadhi ya malengo hayo yalikuwa
ni pamoja na kuwaunganisha wananchi wa Tanganyika na kuwaongoza katika
mapambano ya kupigania uhuru wa nchi yao, kutoa tafsiri mpya ya ukombozi, kuweka
juhudi na fikra mpya za mapambano kwa misingi ya kifalsafa, pamoja na kudai haki
ya kuwa na wawakilishi wa kidemokrasia katika vyombo vya kutunga sheria.
Mbali na chama cha TANU, kulikuwa na vyama vingine vya kisiasa wakati wa
harakati za kupigania uhuru. Mfano wa vyama hivyo ni United Tanganyika Party
(UTP) kilichoanzishwa mwaka 1956, ambacho kiliungwa mkono na Wazungu, Waasia
na baadhi ya Waafrika, hasa machifu. Vyama vingine ni African National Congress
(ANC), kilichojitenga kutoka TANU mwaka 1958 na kuongozwa na Zuberi Mtemvu.
ANC ilipingana na TANU katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika, hasa katika
suala la kupiga kura tatu ambalo mwalimu Nyerere na wanachama wengine wenye
msimamo wa kati walilikubali, huku Zuberi Mtemvu na wanachama wengine wenye
msimamo mkali walilikataa na kuamua kujitenga. Pia, chama cha All Muslim National
Union of Tanganyika (AMNUT) kilikuwa chama cha nne kuanzishwa Tanganyika.
Kama ilivyokuwa TANU, AMNUT pia kilidai uhuru lakini walitaka mabadiliko ya
katiba na uhuru viletwe polepole na si haraka kama TANU ilivyotaka. Mpaka wakati
wa uhuru, Tanganyika ilikuwa na vyama hivi vinne.
Kwa upande wa Zanzibar, vyama vilivyojitokeza kudai uhuru ni pamoja na Zanzibar
Nationalist Party (ZNP) kilichoanzishwa mwaka 1955, Afro-Shirazi Party (ASP)
kilichoanzishwa mwaka 1957 na Zanzibar and Pemba People’s Party (ZPPP)
lililoundwa mwaka 1959. Vyama vyote hivi vilikuwa na lengo kuu la kudai uhuru wa
Wazanzibari, ingawa viliungwa mkono
na wanachama wa rangi tofauti.
Chama cha ASP kiliundwa baada
ya kuunganishwa kwa vyama viwili
vilivyokuwepo hapo awali, yaani African
Association na Shirazi Association. Baada
ya kuundwa kwa chama cha ASP, Sheikh
Abeid Amani Karume alichaguliwa
kuwa Rais wa ASP, Mtoro Rehani Kingo
alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais na
Thabiti Kombo Jecha alichaguliwa kuwa
Katibu Mkuu. Kielelezo 4.6 kinaonesha
picha ya Thabit Kombo Jecha. Kielelezo 4.6: Thabit Kombo Jecha
67
03/10/2024 18:15:16
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 67 03/10/2024 18:15:16
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 67

