Page 73 - Historia_Maadili
P. 73
Kwa upande wa Zanzibar, kulikuwepo na vyombo vya habari kama magazeti na
majarida mbalimbali, kwa mfano, gazeti la Sauti ya Zanzibar (1949), gazeti la
Samachar lililoandikwa na Bwana Mtoro bin Abu Rehan, jarida la African Events na
Alfalaq (1929) lililoandikwa na Ahmed Yahya Aldarda. Magazeti mengine ni Afrika
Kwetu, Muongozo, Jasho Letu, Mkombozi, Mwiba, Sauti ya Afro-Shirazi, Sauti ya
FOR ONLINE READING ONLY
Jogoo na Umma.
Vyombo vya habari vya Waafrika vililenga kuamsha ari ya uzalendo kwa Watanganyika
na Wazanzibari ili kuwaunganisha
katika kudai uhuru wao. Vilikuwa na
jukumu la kutoa elimu ya uzalendo na
kuwaelimisha wananchi kuhusu sera
na itikadi za vyama kama TANU na
ASP. Aidha, vilitumika kuhamasisha na
kupaza sauti dhidi ya maovu yaliyokuwa
yakifanywa na serikali za kikoloni.
Kielelezo 4.4 kinaonesha mojawapo ya
ukurasa wa mbele wa gazeti la Sauti ya
TANU. Kielelezo 4.4: Gazeti la Sauti ya TANU
Vikundi na vyama vya sanaa
Wakati wa utawala wa kikoloni, hakukuwa na nafasi ya kutosha kwa Watanganyika
na Wazanzibari kusimama na kujieleza kwa uhuru kuhusu haki zao na harakati za
ukombozi. Badala yake, mambo mengi
ya harakati za Watanganyika na
Wazanzibari kudai uhuru yalifanyika kwa
siri kuhofia adhabu kutoka kwa wakoloni.
Viongozi na wanachama wa TANU na
ASP waliamua kutumia sanaa na michezo
kama mbinu mbadala.
Sanaa ilitumika katika kukuza na
kuendeleza harakati za kudai uhuru wa
Tanganyika na Zanzibar. Watanganyika Kielelezo 4.5: Bibi Titi Mohamed akiwa
walianzisha vikundi na vyama vya sanaa jukwaani
65
03/10/2024 18:15:15
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 65 03/10/2024 18:15:15
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 65

