Page 71 - Historia_Maadili
P. 71
ukombozi cha Afro-Shirazi Party (ASP) ambacho
pia ndicho kilichoungana na TANU kuunda Chama
Cha Mapinduzi mwaka 1977.
Pamoja na kutetea haki na masilahi ya
wafanyabiashara, vyama hivi vilikuja kushiriki katika
FOR ONLINE READING ONLY
harakati za kudai uhuru, ikiwa ni pamoja na baadhi
yao kubadilika na kuwa vyama vya kisiasa. Kielelezo
4.3 kinaonesha picha ya Abdulwahid Kleist Sykes.
Kielelezo 4.3: Abdulwahid Kleist
Sykes
Vikundi na vyama vya kidini
Dini za Kikristo na Kiislamu zilitumika kama vyombo vya kuwaunganisha watu na
kuendeleza harakati za kudai uhuru wa Tanganyika na Zanzibari. Vyama na vikundi
vya kidini vya Waafrika vilianzishwa kwa lengo la kupigania haki, usawa na uhuru
wa kuabudu, pamoja na kudumisha utamaduni wa Watanganyika na Wazanzibari.
Miongoni mwa vikundi na vyama vya kidini vilivyoanzishwa nchini Tanganyika ni
Al-Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (1933), The Watch Tower Church, The African
National Church na The Church of God.
Al-Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ilitoa viongozi shupavu kama Ally Sykes, Bibi
Titi Mohamed, Tewa Said Tewa na wazalendo wengine ambao baadaye walishirikiana
na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.
Kwa upande wa Zanzibar, kulikuwa na Jumuiya iliyoitwa Jamiyatu Shubbaniul
Muslimin, iliyoanzishwa tarehe 25 Novemba 1935 huko Gulioni, Unguja na Sheikh
Salim Bin Abdullah Al Wadan (1901 - 1941), kwa lengo la kupinga mila na desturi
za Kizungu.
Vilabu vya mpira wa miguu
Vilabu vya mpira wa miguu vya Waafrika vilianzishwa na kusaidia kuimarisha umoja
na mshikamano miongoni mwa Waafrika sambamba na kueneza fikra za ukombozi
dhidi ya madhila ya ukoloni. Vilabu hivyo viliweza kuonesha ushindani mkubwa
dhidi ya vilabu vilivyosimamiwa na wakoloni na hivyo kuamsha ari kwa Waafrika ya
kupambania haki zao za kijamii, kiuchumi na kisiasa. Mwaka 1931 ilianzishwa klabu
ya mpira wa miguu Zanzibar kwa jina la The African Sports Club ambayo kiongozi
wake alikuwa Sheikh Abeid Amani Karume. Aidha, Klabu hii ilikuwa msingi wa
kuanzishwa kwa Jumuiya ya Waafrika (African Association) mwaka 1933 ambayo
iliwaunganisha Waafrika wa Unguja na Pemba kudai haki zao mbalimbali.
63
03/10/2024 18:15:15
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 63 03/10/2024 18:15:15
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 63

