Page 69 - Historia_Maadili
P. 69
Vyama vya wafanyakazi
Waafrika waliokuwa wameajiriwa katika viwanda, mashamba, bandari na sehemu
nyingine walianzisha vyama vyao vya wafanyakazi kwa lengo la kulinda na kutetea
masilahi yao ya kikazi. Malengo hayo yalijumuisha kudai kulipwa mishahara kwa
wakati, ujira unaostahili na mazingira bora ya kazi. Madai mengine yalikuwa ni
FOR ONLINE READING ONLY
kupinga ubaguzi na unyanyasaji kazini, kupunguza masaa au muda wa kazi na kupinga
kodi za kinyonyaji.
Mfano wa vyama hivyo ni Tanganyika Territory Civil Servants’ Association (TTCSA),
kilichoanzishwa na Martin Kayamba mwaka 1922 huko Tanga, ambacho mwaka
1924 kilifungua tawi lake mjini Dar es
Salaam. Pia, ndani ya kipindi hicho cha
mwaka 1922 wafanyakazi wa serikali wa
Dar es Salaam walianzisha Tanganyika
African Government Servants Association
(TAGSA). Vyama vingine vilivyoundwa
ni pamoja na Association of Cooks and
Washmen (1939), Dock Workers’ Union
(1937), Railway African Civil Service Union
(1920) na Tanganyika Federation of Labour
(1955) chini ya uongozi wa Rashid Mfaume
Kawawa. Kielelezo 4.2 kinaonesha picha ya Kielelezo 4.2: Rashid Mfaume
Rashid Mfaume Kawawa. Kawawa
Kwa upande wa Zanzibar, mnamo mwaka 1939, Sheikh Abeid Amani Karume aliunda
Jumuiya ya Mabaharia kwa ajili ya kupigania haki za wafanyakazi katika vyombo
vya baharini. Ambapo mwaka 1941, Jumuiya ya Mabaharia, Jumuiya ya Wachukuzi
na Umoja wa Watumishi wa Nyumba za Wazungu walikutana kujadili mikakati ya
ukombozi dhidi ya unyonyaji kazini. Baadaye, mwaka 1948, Chama cha Masonara,
Chama cha Wafanyakazi wa Hospitali na Chama cha Mafundi wa Majahazi pia
vilikutana kwa lengo la kujadili namna ya kutetea masilahi yao katika sehemu za kazi.
Aidha, Baraza la Umoja wa Vijana wa Kiafrika (Youth African Council Union)
liliundwa mwaka 1949. Baraza hili lilianzishwa kwa madhumuni ya kupigania haki
ya kupata kazi na mishahara inayolingana na elimu na ujuzi wa mtu. Hata hivyo,
mnamo mwaka 1956, Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi wa Zanzibar na Pemba
(Federation of Zanzibar and Pemba Trade Unions - ZPFL) ulianzishwa.
Pamoja na juhudi zao za kutetea masilahi ya wafanyakazi, waliendelea kujadili
masuala ya kisiasa na hatimaye walijihusisha na harakati za kudai uhuru.
61
03/10/2024 18:15:15
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 61 03/10/2024 18:15:15
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 61

