Page 64 - Historia_Maadili
P. 64
Harakati za kudai
Sura ya Nne
uhuru wa Tanganyika
na Zanzibar
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Harakati za kudai uhuru wa Tanganyika na Zanzibar ziliendana na juhudi
mbalimbali za kisiasa na kijamii zilizolenga kukomesha utawala wa kikoloni.
Katika sura hii, utajifunza kuhusu dhana ya uhuru na harakati za kudai uhuru,
pamoja na misingi na mbinu zilizotumika katika kupigania uhuru wa Tanganyika
na Zanzibar. Pia, utajifunza mchango wa harakati hizo katika kuupinga utawala
wa kikoloni, kuyatunza maadili ya Kitanzania na kuujenga uzalendo. Umahiri
utakaoupata utakuwezesha kuthamini juhudi za wapigania uhuru wa Tanganyika
na Zanzibar na pia kuuheshimu na kuuenzi uhuru wetu.
Fikiri
Harakati za kudai uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Dhana ya uhuru na harakati za kudai uhuru
Neno “uhuru” linaweza kufafanuliwa kwa namna mbalimbali. Uhuru ni hali ya mtu
au nchi kuamua na kufanya mambo yake bila kuingiliwa na mtu au taifa lolote, iwe
kiuchumi, kisiasa, kijamii au kiutamaduni. Katika muktadha huu, uhuru ni hali ya nchi
kujikomboa kutoka kwenye ukoloni wa mataifa ya kibepari. Harakati za kudai uhuru
wa Tanganyika na Zanzibar ni mchakato au juhudi za watu wa nchi hizo kutafuta
uhuru kutoka kwa serikali za kikoloni. Pia, ni hatua zilizochukuliwa na wananchi wa
Tanganyika na Zanzibar hadi kufanikisha kupata uhuru wao.
Tanganyika ilitawaliwa na wakoloni wa Kijerumani kuanzia mwaka 1885 hadi 1918.
Baada ya Vita ya Kwanza vya Dunia, Tanganyika ilitawaliwa na Waingereza hadi
ilipopata uhuru wake tarehe 9 Desemba, 1961. Zanzibar ilikuwa chini ya utawala
wa Kisultani kutoka Oman kuanzia mwaka 1840 hadi 1890, kisha ikatawaliwa
na Waingereza kuanzia mwaka 1890 hadi 1963. Baada ya harakati za kutafuta
uhuru,Waingereza walikabidhi uhuru wa Zanzibar kwa vyama vya ZNP na ZPPP
56
03/10/2024 18:15:14
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 56 03/10/2024 18:15:14
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 56

