Page 60 - Historia_Maadili
P. 60
wavamizi kama Wajerumani baadae. Lakini baadae mpango wao ulishindwa na wao
kujikuta wakitawaliwa kirahisi zaidi. Mfano wa jamii hizi za Kitanzania ni kama vile
Wachaga. Ambao chini ya Mangi Mandara waliungana na Wajerumani ili kumshinda
Mangi Sina; Mangi Marealle aliungana na Wajerumani ili kumshinda Mangi Meli;
Wasangu na Wabena chini ya Mtwa Merere na Mbeyela mtawalia waliungana na
Wajerumani dhidi ya Wahehe chini ya Mtwa Mkwawa na jamii zingine nyingi.
FOR ONLINE READING ONLY
Ukweli ni kwamba jamii hizi zote zilishindwa kupata walichokitarajia na mwisho
kutawaliwa kirahisi sana na Wajerumani. Hivyo, usaliti wao dhidi ya watawala wa
jamii za Kitanzania kwa kuungana na wakoloni Wakijerumani ulikuwa ni fedheha
kwao kwani haukuwa na manufaa yoyote.
Kwa njia ya kusalimu amri
Kuna baadhi ya jamii za Kitanzania ambazo hazikupenda kutawaliwa na wakoloni
lakini zilijiona hazina uwezo wa kuweza kukabiliana na Wajerumani kivita. Nyingi
ya jamii hizi ni zile zilizokuwa zimeathirika na baa la njaa au magonjwa, ukosefu
wa dola zenye nguvu mazingira magumu ya kivita na sifa nyingine kama hizo. Kwa
mfano, jamii ya Kimasai hapa nchini ilisalimu amri kwa Wajerumani kufuatia kupatwa
na majanga ya magonjwa ya Wanyama miaka ya 1870s na 1880s na mazingira yake
kutokuwa mazuri kwa vita.
Zoezi la 3.3
1. Fafanua namna jamii za Watanzania na viongozi wao walivyoupinga utawala
wa Wajerumani.
2. Eleza mbinu zinazoweza kutumiwa na jamii za sasa za Kitanzania kulinda
rasilimali, utamaduni na maadili ya jamii zao.
3. Eleza kwa nini vita ya Maji Maji hujulikana kama vita kubwa Tanzania.
Changamoto zilizokabili mapambano dhidi ya uvamizi wa kikoloni
Wananchi walijaribu kupambana na kupinga ukoloni, lakini wakoloni waliwazidi
nguvu na kuwashinda. Zipo sababu nyingi zilizowafanya wananchi kushindwa katika
mapambano hayo. Miongoni mwa sababu hizo ni kama zinavyoelezwa katika sehemu
zinazofuata.
Ukosefu wa umoja miongoni mwa jamii za Kitanzania
Kama ilivyoonekana, mapambano dhidi ya ukoloni yalifanywa kati ya wakoloni na
jamii moja moja za Kitanzania. Hii inamaanisha kuwa, katika kipindi cha ukoloni,
jamii za Kitanzania zilishindwa kwa sababu zilikosa umoja na hazikushirikiana
kupambana na wakoloni. Kwa mfano, hata katika vita ya Maji Maji, makabila
hayakuungana yote kwa pamoja kila kabila lilipigana kivyake katika eneo lake.
52
03/10/2024 18:15:14
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 52 03/10/2024 18:15:14
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI F2.indd 52

